Facebook

Sunday 24 August 2014

Wachimba migodi wafariki Afrika ya Kati.

Rais Samba-Panza wa Jamhuri ya Afrika ya Kati na waziri mkuu wake, Mahamat Kamoun mjini Bangui
Wakuu wa Jamhuri wa Afrika ya Kati wanasema watu kama 20 wamekufa kwenye mgodi wa dhahabu karibu na mji wa Bambari.
Mgodi huo ni wa kampuni ya Canada, lakini ulitekwa na wapiganaji wa Seleka zaidi ya mwaka mmoja uliopita na sasa umo katika uchumi wa kimagendo ambao unagharimia ghasia za kidini baina ya
Seleka, Waislamu, na makundi ya Wakristo ya anti-Balaka.
Na Waziri Mkuu mpya wa nchi hiyo, Mahamat Kamoun, ameteua baraza lake jipya la mawaziri, wakiwemo wajumbe kutoka makundi hayo mawili ya wapiganaji.
Rais wa mpito, Catherine Samba-Panza, amekariri kwamba anaamini kuwa Bwana Kamoun ana uwezo wa kuongoza nchi hadi uchaguzi wa mwaka ujao.
Kikosi cha Umoja wa Mataifa kinatarajiwa kushika kazi ya kuweka amani nchini humo kutoka mwezi ujao.

0 comments:

Post a Comment