Ripoti kutoka Yemen zinasema
kuwa kumekuwa na vita vikali kati ya jeshi la taifa hilo na waasi wa
ki-shia kazkazini mwa taifa hilo kufuatia kuvunjwa kwa mkataba wa
kusitisha vita uliowekwa mwezi uliopita.
Ripoti moja iliowanukuu maafisa wa eneo hilo
imesema kuwa jeshi la angani liliwashambulia waasi hao wanaojulikana
kama Houthi siku ya jumamosi na kwamba takriban watu 70 waliuawa.Pande zote mbili zili-laumiana kwa kuvunja makubaliano hayo ya kusitisha vita.
Waandishi wanasema kuwa migogoro ya kidini pamoja na hatua za kuimarisha uhuru wa kikanda ndani ya Yemeni umekandamiza maridhiano ya kitaifa.
0 comments:
Post a Comment