Facebook

Sunday, 6 July 2014

James Rodriguez afunguka kuhusu kutokwa na machozi.


James Rodriguez amesisitiza kwamba alishindwa kuvumilia machungu aliyoyapata mara baada ya kutolewa katika michuano ya Kombe la Dunia katika hatua ya robo fainali ukizingatia walivyo wakicheza kwa kujituma,aliendelea kusisitiza kuwa walistahili kushinda mchezo huo wajana.
Mchezaji huyu mwenye umri wa miaka 22,aliendelea kufunguka kuwa wanaume pia kuna wakati mwingine hutokwa na machozi kwani na wenyewe ni binadamu,na wanayomapungufu yao,hivyo haoni kama swala la yeye kutokwa na machozi baada ya filimbi ya mwisho ni kama kitendo cha ajabu.
Aliendelea kusema kuwa alifurahishwa na kitendo cha David Luiz kumfata na kumpa maneno ya faraja mara baada ya mechi kuisha.
Nafsi zetu zilijawa nahuzuni kubwa kwa sababu dhamira yetu ilikuwa ni kusonga mbele katika michuano hii na kutengeneza rekodi mpya na timu yetu ya Colombia.Alisikika James Rodriguez wakati akifanya mahojiano na waandishi wa habari.

Related Posts:

0 comments:

Post a Comment