Facebook

Saturday, 5 July 2014

Neymar kukosa kombe la dunia

Mchezaji Neymar baada ya kupata jeraha
Nyota wa timu ya soka ya Brazil Neymar hatoshiriki tena katika michuano ya kombe la dunia baada kupata jeraha.
Mfupa wake unaoshikana na uti wa mgongo ilivunjika katika mechi ya ushindi wa mabao mawili dhidi ya Colombia.
Neymar aligongwa upande wake wa nyuma dakika tano tu kabla ya mchuano huo wa robo fainali kukamilika.
Alibebwa na kutolewa nje akiwa katika machela lakini ametolewa hospitalini baada ya kufanyiwa matibabu.
Brazil pia itaendelea kushiriki katika mashindano hayo bila nahodha wake Thiago Silva katika mchuano wa nusu fainali dhidi ya Ujerumani baada ya mchezaji huyo kupewa kadi ya pili ya Njano.
Kabla ya habari hizo za Neymar kutolewa raia wa Brazil walifurika katika barabara za taifa hilo kusherehekea ushindi wa timu yao.
Katika robo fainali ya kwanza Ujerumani iliishinda ufaransa kwa bao moja kwa bila .

Related Posts:

  • Hispania yaaga kombe la dunia Brazil. Kufuatia ushindi huu wa mabao 2-0 mikononi mwa Chile mabingwa watetezi wa kombe la dunia Uhispania sasa wamehakiki tikiti za ndege kurejea nyumbani pam… Read More
  • Ujerumani yaifumua Ureno bila huruma, Thomas Mueller ndiye mchezaji wa kwanza kufunga mabao matatu katika mechi moja Brazil Thomas Muller alifunga mabao matatu na kuisaidia Ujerumani kuishinda Ureno mabao manne kwa nunge. Mlinzi wa U… Read More
  • Marekani yaifumua Ghana 2-1 Marekani yalipiza kisasi cha kushindwa na Ghana 2-1katika kombe la dunia Bao la kichwa la John Brooks, katika dakika za mwisho za mechi ziliisaidia Marekani kuilaza Ghana kwa mabao mawili kwa moja, katika mchuan… Read More
  • Nigeria na Iran zatoka sare. Timu ya Iran na Nigeria zilitoka sare ya suluhu bin suluhu , katika mechi yao ya kundi F huko Curitiba, kwenye fainali ya kombe la dunia siku ya Jumatatu. Timu hiyo ya Carlos Queiroz ilioneka… Read More
  • Rooney katika mgogoro mzito Brazil Wayne Rooney achezeshwe katika nafasi gani ? Njama dhidi ya Wayne Rooney yaweza kuhatarisha matarajio yao katika kombe la dunia. Frank Lampard ameonya. Uc… Read More

0 comments:

Post a Comment