Mshambuliaji wa Liverpool Luis Suarez anatarajiwa kukamilisha uhamisho
wake wa pauni milioni 80 kwenda Barcelona katika saa 48 zijazo (Daily
Mail),
Dau la Liverpool la pauni milioni 20 la kumtaka beki Dejan
Lovren limekataliwa na Southampton (Liverpool Echo),
Manchester United
wamepewa Angel Di Maria na Real Madrid kwa pauni milioni 40. Arsenal,
Paris St-Germain na Juventus pia wanamtaka pia mchezaji huyo wa
kimataifa wa Argentina (Daily Star),
Meneja wa Arsenal, Arsene Wenger
ana uhakika wa kuwasajili Alexis Sanchez na Mathieu Debuchy kwa pauni
milioni 35 (Daily Mirror),
Washika bunduki hao pia watatoa dau la pauni
milioni 20 kwa Southampton kumsajili Morgan Schneiderlin, ambaye
anasakwa pia na Napoli (Daily Express),
Bayern Munich huenda wakawazidi
kete Manchester United, Liverpool na Arsenal kumchukua winga wa
Fiorentina, Juan Cuadrado (Daily Express),
Arsenal pia wametoa dau la
pauni milioni 23.8 kumwania kiungo wa Real Madrid, Sami Khedira na
watamtumia rafiki yake wa karibu Mesut Ozil kumshawishi (Metro),
Dau la
pauni milioni 32 la Manchester City kumtaka beki Eliaquim Mangala
limekubaliwa na Porto, lakini bado wanasubiri kama Chelsea nao pia
watapanda dau (Daily Star),
Juventus wako makini kumsajili beki wa
Manchester United Patrice Evra, ambaye amesaini mkataba mpya Old
Trafford mwezi uliopita (Talksport),
Barcelona wataajiri mwanasaikolojia
wa kumsaidia Luis Suarez kukabiliana na 'mizimu' atakapokamilisha
uhamisho wake (Sun)
QPR wanatarajia kukamilisha usajili wa Rio Ferdinand
wiki ijayo (Get WestLondon),
kipa wa Chelsea Petr Cech huenda
akaondoka Darajani kabla ya msimu mpya kuanza, kwa mujibu wa wakala wake
(Talksport).
Share tetesi hizi na wapenda soka wote. Tetesi nyingine
kesho tukijaaliwa.
Endelea kutembelea www.bantutz.com uweze kupata tetesi mbalimbali za usajili kutoka katika vyanzo mbalimbali sisi tutakukusanyia na utapata tetesi zote hapa kwa muda na wakati muafaka.
0 comments:
Post a Comment