Mcheza
filamu Zohra Sehgal wa India, maarufu kama mkongwe wa Bollywood,
amefariki dunia mjini Delhi akiwa na umri wa miaka 102.
Mkongwe huyo
alianza fani yake kama mcheza dansi na baadaye kuingia katika uigizaji
ambapo alijipatia tuzo kadhaa katika
filamu za Bollywood. Katika miaka ya 1960 alihamia London ambapo aliishi
kwa miaka 30 kabla ya kurejea India.
Filamu ambazo ametajwa za
Hollywood na za Uingereza ni: Never Say Die, Bend It Like Beckham, The
Jewel in the Crown, My Beautiful Laundrette na Bhaji on the Beach.
0 comments:
Post a Comment