Kocha wa Uholanzi Louis van Gaal amesema kumaliza Kombe la Dunia kwa kucheza kutafuta nafasi ya tatu "si haki".
Mholanzi huyo, ambaye timu yake ilipoteza kwa Argentina kwa mikwaju ya penati, atakabiliana na Brazil siku ya Jumamosi kutafuta mshindi wa nafasi ya tatu.
"Mechi hii haitakiwi kabisa kuchezwa. Nimekuwa nikisema hilo kwa miaka 10 sasa; sio haki," amesema Van Gaal, ambaye ataanza kuifundisha Manchester United msimu ujao.
"Kuna zawadi moja tu yenye maana, na hiyo ni kuwa mabingwa wa dunia."

0 comments:
Post a Comment