Msemaji wa mwanariadha wa Afrika Kusini anayetuhumiwa kwa mauaji, Oscar Pistorius amesema mwanamichezo huyo alifarakana na mtu mmoja kwenye ukumbi wa starehe mwishoni mwa wiki.
Mtafaruku huo ulikuwa kati yake na mfanyabiashara Jared Mortimer katika klabu ya usiku jijini Johannesburg, limeripoti gazeti la The Star.
Msemaji wa familia yake amesema wawili hao walizozana baada ya bwana Mortimer kuanza "kumhoji vikali" kuhusiana na kesi yake ya mauaji.
Bwana Pistorius anakana kumuua mpenzi wake Reeva Steenkamp.
Anasema alidhani ni mwizi ameingia nyumbani kwake, lakini waendesha mashtaka wanasema alimpiga risasi makusudi baada ya kukorofishana naye.
Bi Steenkamp aliuawa nyumbani kwa bwana Pistorius mjini Pretoria Februari 14 2013.
0 comments:
Post a Comment