Israel imekubali pendekezo la Misri la kutuliza mapigano katika mzozo wa Gaza.
Hamas, inayodhibiti Gaza haijajibu rasmi, lakini tawi lake la kijeshi limetupilia mbali mpango huo likisema ni kama "kujisalimisha".
Chini ya mpango huo, mapigano yatasitishwa mara moja, na kufuatiwa na mfululizo wa mazungumzo ya ngazi ya juu mjini Cairo na wajumbe kutoka pande zote mbili.
Maafisa wa Palestina wanasema watu wasiopungua 192 wameuawa na mashambulio ya anga ya Israel yaliyoanza siku nane zilizopita, kuzuia maroketi yanayoelekezwa Israel.
Kumekuwa hakuna mashambulio ya anga kutoka Israel kwenda Gaza tangu saa tatu asubuhi saa za huko ambao ni muda uliopendekezwa wa kusimamisha mapigano, lakini kumekuwa na roketi moja iliyorushwa kwenda Israel.
0 comments:
Post a Comment