Polisi mmoja nchini Uganda imeripotiwa amempiga risasi na kumuua kobe mmoja baada ya kudai "alishambuliwa vikali" na mnyama huyo.
Tukio hilo lilitokea katika wilaya ya Nebbi, kaskazini mwa Uganda karibu na mpaka na Jamhuri ya Kidemokrasi ya Kongo. kwa mujibu wa gazeti la New Vision afisa huyo, Charles Onegiu alisema kobe huyo aliingia nyumbani kwake na kumshambulia wakati akiwa amekaa anakunywa chai.
"Nilijaribu kumtisha,
lakini kobe huyo akawa mkali sana. Nilichukua fimbo na kumfukuza, lakini
badala yake akaanza ghasia," polisi huyo ameliambia New Vision. Baada
ya kujaribu kumfukuza kwa kutumia kiti cha plastiki, amesema alitoa
bunduki yake na kumpiga risasi. Kundi moja la kidini lilimuombea afande
Onegiu kabla ya kumchoma moto kobe.
Kamanda wa polisi wa wilaya ya Nebbi
Onesmus Mwesigwa alipoulizwa kuhusu jambo hilo amesema huenda shambulio
hilo limetokana na imani za kishirikina, akisema watu hufikiri "kuna
mtu ananitafuta". Kamanda Mwesigwa amewataka wananchi wa eneo hilo kuwa
watulivu, limesema New Vision.
0 comments:
Post a Comment