Manchester City wamemsajili kipa wa Malaga Willy Caballero. Muargentina huyo mwenye umri wa miaka 32, amesaini mkataba wa miaka mitatu kwa kitita ambacho hakikutajwa.
Caballero, aliyecheza chini ya Manuel
Pellegrini wakati akiwa Malaga, alikuwa
jijini Manchester siku ya Jumatatu kwa ajili ya vipimo vya afya.
Anakuwa
mchezaji wa tatu kusajiliwa na mabingwa wa England, baada ya Fernando
kutoka Porto na beki wa zamani wa Arsenal, Bacary Sagna. Caballero
anatarajiwa kuwa kipa wa akiba na pia kutoa changamoto wa kipa namba
moja wa Englad Joe Hart.
0 comments:
Post a Comment