Facebook

Monday, 14 July 2014

Simanzi yatawala baada ya mfanyabiashara maarufu kuawa Mombasa.

 Photo: MFANYABIASHARA MAARUFU AUAWA MOMBASA
Watu wawili wenye bunduki wamemuua mfanyabiashara maarufu mjini Mombasa anayeshtakiwa kwa ugaidi nchini Kenya.
Mohamed Shahid Butt alikuwa ndani ya gari lake akitokea kwenye uwanja wa ndege siku ya Ijumaa, ambapo gari lake lilizuiwa na gari jingine kabla ya watu wawili kumpiga risasi.
Bwana Butt alikuwa afike mahakamani mwezi ujao kujibu mashtaka ya tuhuma za kufadhili itikadi kali kwa vijana wa Kiislam. 
Kumekuwa na mfululizo wa mauaji ya watu wanaodaiwa kujihusisha na Uislam wenye itikadi kali katika eneo la pwani karibu na Mombasa. 
Wanaharakati wa haki za binaadam wameituhumu serikali ya Kenya kwa kuhusika na mauaji hayo, kwa kuwa kesi chache zimeweza kushughulikiwa. 
Mkuu wa polisi wa kaunti ya Mombasa, Richard Kitur, ameliambia shirika la habari la Associated Press kuwa bwana Butt alikuwa ametoka kumpokea mwanaye wa kiume kutoka uwanja wa ndege, kabla hajapigwa risasi. 
Bwana Butt alifikishwa mahakamani mwaka jana akituhumiwa na mamlaka kwa uchochezi na kufadhili shughuli za kigaidi.
Katika miaka miwili iliyopita, Waislam watatu wanaofahamika sana, na ambao walikuwa wakijulikana kujihusisha na itikadi kali wameuawa. 
(Picha- KTN)

Related Posts:

  • Ebola yaanza kuonekana Ghana.    Ghana inatibu mtu mmoja anayedhaniwa kuwa na Ebola, kwa mujibu wa wizara ya afya. Ebola imesababisha vifo vya zaidi ya watu 460 mpaka sasa tangu ugonjwa huo ulipoanza nchini Guinea mwezi Februari, na kusam… Read More
  • Israel: Tumewakamata washukiwa wa mauaji Taarifa kutoka nchini Israeli zinasema kuwa serikali inawazuia baadhi ya watu kwa tuhuma za kuhusika na mauaji ya kijana wa kipalestina… Read More
  • Mamia wateketea na Ebola Afrika Magharibi.   Maafisa wa afya wa Afrika Magharibi wanasema watu 25 zaidi wamekufa kutokana na maradhi ya Ebola tangu Julai 3, na kusababisha idadi ya waliokufa hadi sasa kufikia 518. Shirika la Afya Duniani (WHO) limesema … Read More
  • Tufani kubwa na lenye nguvu laelekea Japan.     Maelfu ya watu wametakiwa kutafuta hifadhi salama wakati tufani lenye nguvu likipita katika kisiwa cha Okinawa nchini Japan. Tufani hilo lililopewa jina la Neoguri lilotarajiwa kukatisha katika kisiwa cha… Read More
  • Wasichana 60 waliotekwa na Boko Haram Watoroka.    Zaidi ya wanawake na wasichana 60 wameripotowa kutoroka kutoka katika kundi la Boko Haram, kwa mujibu wa vyanzo vya kiusalama. Wanawake na wasichana hao ni miongoni mwa 68 waliotekwa mwezi uliopita karibu na… Read More

0 comments:

Post a Comment