Juventus wanajipanga kutoa pauni milioni 20 kumchukua Paulinho, 25, kutoka Tottenham, hatua hiyo huenda ikatoa mwanya
kwa Manchester United kumchukua Arturo Vidal, 27 (Sunday Telegraph),
Winga wa Real Madrid Angel Di Maria, 27, huenda akakataa kwenda
Manchester United licha ya kupewa mshahara wa 150,000 kwa wiki (Daily
Express),
Mshambuliaji wa Ecuador Enner Valencia, 25, amewasili London
kukamilisha uhamisho wake kwenda West Ham kutoka klabu ya Pachuca ya
Mexico (The Sun on Sunday),
Manchester City wanakaribia kumsajili beki
wa kati wa Ufaransa Eliaquim Mangala, ambaye Manuel Pellegrini anaamini
atacheza vyema na Vincent Kompany (Mail on Sunday),
Meneja mpya wa
Manchester United Louis van Gaal, ambaye huenda akaingia rasmi Old
Trafford siku ya Alhamisi, anatarajia kuwasajili Mats Hummels na Marco
Reus (Sunday Express),
Van Gaal, 62, pia amemwambia winga Arjen Robben
kuwa anakaribishwa Old Trafford (Sunday Telegraph),
Liverpool
wanajiandaa kutoa pauni milioni 26 kumsajili Romelu Lukaku, 21, kutoka
Chelsea (Caughtoffside.com),
Newcastle imewasiliana na Monaco kujaribu
kumsajili mshambuliaji Emmanuel Reviere, 24 (Sunday Mirror),
AC Milan
wamesema hawatomsajili tena beki Sime Vrsaljiko ambaye anasakwa na
Arsenal (Talksport),
Dynamo Moscow wanataka kumchukua Wilfired Zaha, 21,
kutoka Manchester United baada ya kumchukua Alex Buttner (Sun on
Sunday),
Beki wa kati wa Roma Mehdi Benatia anataka kuhamia Chelsea
(Gazetta dello Sport),
Barcelona wanamtazama kwa karibu beki wa
Tottenham Jan Vertonghen. Barca pia wanamfuatilia Mats Hummels wa
Borussia Dortmund (Mundo Deportivo),
Mshambuliaji wa Manchester United
Bebe amefikia makubaliano na Benfica ya uhamisho wa kudumu. Klabu hizo
mbili bado hazijakubaliana bado kuhusu ada (A Bola),
Angel Di Maria
angependa kwenda Paris Saint-Germain badala ya Manchester United ambayo
haichezi Champions League msimu ujao (Sunday Times),
Mourinho
huenda akamchukua Javier Pastore kutoka PSG kwa pauni milioni 25 iwapo
mabingwa hao wa Ufaransa watamchukua Angel Di Maria (Daily Express),
Licha ya kununua wachezaji watatu mpaka sasa, boss wa Liverpool Brendan
Rodgers anataka kununua wachezaji wengine sita. Rodgers ameambiwa
anaweza kutumia kitita chote cha kumuuza Luis Siarez, na henda akatumia
hadi pauni milioni 135 (Sunday People),
Luis Suarez huenda akakatwa
pauni milioni 3 katika mshahara wake wa pauni milioni 10 kwa mwaka ikiwa
atamng'ata mchezaji mwingine akiwa Barcelona (Sunday People).
Share
tetesi hizi na wapenda soka wote. Tetesi nyingine kesho tukijaaliwa.
Cheers!
0 comments:
Post a Comment