Liverpool imesema haikuhusika na chochote kuhusiana na hatua ya kuomba radhi ya Luis Suarez baada ya kumng'ata Giorgio Chiellini, ili kusaidia uhamisho wake kwenda Barcelona (Independent),
Meneja wa Arsenal, Arsene
Wenger anapanga kutoa pauni milioni 23
kumchukua kiungo wa Real Madrid Sami Khedira ili kumsaidia Mesut Ozil
(Sun),
Atletico Madrid wanajiandaa kutoa pauni milioni 20 kumchukua
mshambuliaji wa Manchester City Alvaro Negredo (Daily Star),
Manchester
City wanamtaka kipa wa Malaga Willy Caballero ili kutoa ushindani kwa
Joe Hart (Daily Mail),
Arsenal na Liverpool wanamfuatilia kwa karibu
kipa wa Costa Rica, Keylor Navas anayechezea Lavante, lakini ana kifungu
cha kuzuia ununuzi cha pauni milioni 6.5 (Daily Mirror),
Tottenham
wanapambana na Arsenal kumsaka beki wa kulia wa Toulouse Serge Aurier
raia wa Ivory Coast (Daily Mail),
Kiungo wa Chile Arturo Vidal amedokeza
kuwa angependa kwenda Old Trafford kuliko klabu nyingine (Daily Star),
Mshambuliaji wa Chile, Alexis Sanches anataka kusalia Barcelona msimu
ujao, lakini inadaiwa angependa kwenda Arsenal au Liverpool iwapo
atalazimishwa kuondoka (Metro),
Beki wa kushoto wa Brazil Filipe Luis
anataka sana kwenda Chelsea kiasi kwamba amekata mawasiliano yote na
klabu yake ya Atletico Madrid (Daily Express),
Arsenal wamekataliwa ombi
lao kuhusu kiungo wa Roma Alessandro Florenzi (Metro). Tetesi nyingine
kesho tukijaaliwa.
Endelea kutembelea www.bantutz.com kupata tetesi mbalimbali za usajili katika kipindi hiki cha usajili barani Ulaya.
0 comments:
Post a Comment