Facebook

Wednesday, 16 July 2014

Tetesi za usajili katika magazeti mbalimbali barani Ulaya.


Salim Kikeke's photo. Kiungo wa Juventus Arturo Vidal, 27, amewapa matumaini zaidi Manchester United baada ya kukiri kuwa "angependa kuichezea moja ya klabu kubwa duniani" ingawa amesema hatolazimisha uhamisho wake (Independent) United pia wamepata matumaini baada ya winga wa Real Madrid, Angel Di Maria, 26, kukataa kwenda Paris St- Germain (Daily Mirror),

 Beki wa Atlètico Madrid, Filipe Luis, 28, anajiandaa kufanya vipimo vya afya kabla ya kuhamia Chelsea kwa ada ya pauni milioni 20 (Daily Express), 

Boss wa Sevilla Unai Emery amesema anajiandaa kumpoteza beki wake wa kushoto Alberto Moreno, 22, ambaye anasakwa na Liverpool (Talksport)
 Salim Kikeke's photo.
Mshambuliaji wa Paris St-Germain Edison Cavani, 27, amemtaka wakala wake kumtafutia timu katika Ligi Kuu ya England (Sky Sports), 

Arsenal wapo tayari kuacha kumfuatilia kiungo wa Real Madrid Sami Khedira, 27, kufuatia kudai mshahara mkubwa. Khedira anataka kuwa mchezaji anayelipwa zaidi Emirates (Daily Mirror), 

Arsenal wanaongeza ufuatiliaji wa beki wa kulia wa Southampton Calum Chambers, 19, licha ya kuwa wanakaribia kumchukua Mathieu Bebuchy, 28, kutoka Newcastle (Daily Mail),

Beki wa zamani wa Manchester. United Rio Ferdinand, 35, atasaini kuichezea QPR siku ya Jumanne (Sky Sports),

 Liverpool huenda wakipanda dau la pauni milioni 44 kumtaka mshambuliaji wa Borussia Dortmund Marco Reus, 25, (Daily Express), 

Dynamo Moscow wamekubaliana na Marseille kumsajili Mathieu Valbuena, 29, kwa pauni milioni 5.5. Arsenal, Tottenham na West Ham zilikuwa zikimtaka pia (Talksport), 

Robin Van Persie amepewa wiki tatu za kupumzika na Manchester United baada ya Kombe la Dunia, huku Wayne Rooney wa Engalnd akitakiwa kuripoti kambini mapema (Sun), 
 Salim Kikeke's photo.
kiungo wa Arsenal Jack Wilshire, 22, aliyeomba radhi mwezi Oktoba kwa kuonekana akivuta sigara, ameonekana tena akifanya hivyo mjini Las Vegas akiwa na Joe Hart (Daily Mail),
 
Arsenal watataka Chris Smalling kujumuishwa kwenye mkataba wowote iwapo Manchester United watamchukua Thomas Vermaelen (Metro) 

Newcastle wamekamilisha usajili wa Daryl Janmaat wa pauni milioni 5, kuziba nafasi ya Mathieu Debuchy (Guardian).

 Share tetesi na wapenda soka. Tetesi nyingine kesho tukijaaliwa. Cheers!

Related Posts:

  • Mbeya City yafungua ukurasa wa usajili.Mshambuliaji wa kutumainiwa wa Ndanda Fc, Gideon Benson amesaini kandarasi ya mwaka mmoja na nusu kujiunga na kikosi ch Mbeya City fc kinachonolewa na Juma Mwambusi katika msimu ujao Benson ameweka kando ofa kadhaa aliz… Read More
  • Singano "Messi" katika mtihani mzito Msimbazi. SIMBA SC inajipanga kumchukulia hatua mchezaji wake, Ramadhani Singano ‘Messi’ kwa kuituhumu klabu hiyo kughushi Mkataba wake. Mkuu wa Idara ya Habari na Mawasiliano ya Simba SC, Hajji Sunday Manara ‘Zungu’ amefanya Mkut… Read More
  • Tetesi zote za Usajili wa wachezaji barani Ulaya siku ya leo.Dau la Manchester United la pauni milioni 110 kwa Real Madrid kumtaka Gareth Bale, 25 na beki Rafael Varane, 22 limekataliwa na klabu hiyo ya La Liga (Daily Express),   Real Madrid wana uhakika wa kumsajili kwa pauni m… Read More
  • Man City yamnyatia Isco.Manchester City inataka kupata saini ya kiungo wa Real Madrid Isco. Mchezaji huyo miaka 23 hajui hatima yake Santiago Bernabeu baada ya ujio wa meneja mpya Rafa Benitez.Isco alijiunga na Real Madrid kwa ada ya Euro milioni30 … Read More
  • Chelsea yarusha ndoano kwa Gundogan.Timu ya chelsea inatajwa katika mbio za kuhitaji saini ya mchezaji IIkay Gundogan kutoka Dortmund lakini taarifa zinasema mchezaji huyo yupo katika mazungumzo na vilabu vingine vya Barcelona, Manchester United.Bayern na Ars… Read More

0 comments:

Post a Comment