
Bingwa wa zamani wa mbio za mita 100 Asafa Powell na Sherone Simpson wote kutoka Jamaica wamepunguziwa adhabu ya kufungiwa, kutoka miezi 18 hadi miezi sita.
Uamuzi uliotolewa na mahakama ya usuluhisi wa michezo (Cas), unamaanisha wanariadha hao wako huru kuanza kushiriki mashindano mara moja. Powell atashiriki mbio za Lucerene nchini Uswisi siku ya Jumanne.
Wawili hao walikuwa na ruhusa ya kushiriki mashindano yoyote tangu Juni 18 wakati wakisubiri uamuzi wa rufaa yao.
Vipimo kwa wanariadha hao vilikuta wakitumia dawa ya kuongeza nguvu ya oxilofrine iliyopigwa marufuku mwaka jana wakati wakishirini michuano ya taifa ya Jamaica.
0 comments:
Post a Comment