Facebook

Monday, 14 July 2014

Tiketi za Manchester United zashambuliwa kwa nguvu.

 Photo: MANCHESTER UNITED imetangaza kuwa Tiketi zote 55,000 za kuingia kwenye Mechi Uwanjani Old Trafford kwa Msimu mzima zimeuzwa na hii imevunja Rekodi ya Tiketi za Msimu kumalizika mapema.
OLD_TRAFFORDbestWachambuzi wanadai kuuzwa huko kwa Tiketi hizo haraka tangu Old Trafford ilipopanuliwa na kuwa ya Viti 76,000 Mwaka 2006 kumekuja hasa kutokana na shauku ya Mashabiki baada ya Meneja wao mpya Louis van Gaal kufanya vizuri huko Brazil akiwa na Netherlands na kuifikisha Nusu Fainali ya Kombe la Dunia.
Baada kuuzwa Tiketi hizo 55,000 Tiketi zilizobaki 21,000 huwekwa pembeni kwa makusudi na rasmi kwa ajili ya Mashabiki wa Timu za Ugenini na kwa Mashabiki wanaotaka kuhudhuria baadhi ya Mechi na si Mechi zote za Msimu wote.
Watu wengi walihofia kuwa baada ya Man United kufanya vibaya Msimu uliopita chini ya David Moyes na kumaliza Ligi wakiwa Nafasi ya 7 na hivyo kukosa kabisa kucheza Mashindano ya Klabu Ulaya kungeweza kuathiri mahudhurio ya Watazamaji Old Trafford.
Lakini hali imekuwa tofauti hasa baada ya kumtangaza Louis van Gaal Meneja mpya ambae anatarajiwa kutambulishwa rasmi huko Old Trafford Alhamisi kabla Ijumaa kuruka kwenda Marekani kwa Ziara Kabla Msimu Mpya Kuanza.
MANCHESTER UNITED imetangaza kuwa Tiketi zote 55,000 za kuingia kwenye Mechi Uwanjani Old Trafford kwa Msimu mzima zimeuzwa na hii imevunja Rekodi ya Tiketi za Msimu kumalizika mapema.
Wachambuzi wanadai kuuzwa huko kwa Tiketi hizo haraka tangu Old Trafford ilipopanuliwa na kuwa ya Viti 76,000 Mwaka 2006 kumekuja hasa kutokana na shauku ya Mashabiki baada ya Meneja wao mpya Louis van Gaal kufanya vizuri huko Brazil akiwa na Netherlands na kuifikisha Nusu Fainali ya Kombe la Dunia.

Baada kuuzwa Tiketi hizo 55,000 Tiketi zilizobaki 21,000 huwekwa pembeni kwa makusudi na rasmi kwa ajili ya Mashabiki wa Timu za Ugenini na kwa Mashabiki wanaotaka kuhudhuria baadhi ya Mechi na si Mechi zote za Msimu wote.
Watu wengi walihofia kuwa baada ya Man United kufanya vibaya Msimu uliopita chini ya David Moyes na kumaliza Ligi wakiwa Nafasi ya 7 na hivyo kukosa kabisa kucheza Mashindano ya Klabu Ulaya kungeweza kuathiri mahudhurio ya Watazamaji Old Trafford.
Lakini hali imekuwa tofauti hasa baada ya kumtangaza Louis van Gaal Meneja mpya ambae anatarajiwa kutambulishwa rasmi huko Old Trafford Alhamisi kabla Ijumaa kuruka kwenda Marekani kwa Ziara Kabla Msimu Mpya Kuanza.

Related Posts:

0 comments:

Post a Comment