Ushindi wa Ujerumani wa 7-1 dhidi ya Brazil katika nusu fainali ya
Kombe la Dunia umekuwa gumzo kubwa. Mchezo huo umekuwa jambo la
kimichezo lililojadiliwa zaidi kwenye mtandao wa Twitter mpaka
sasa.
Takriban tweets milioni 35.6 zilitumwa katika kipindi cha dakika
90 za mchezo huo, na kuvunja rekodi ya dunia. Pia ilivunja rekodi ya
tweets kutumwa katika dakika moja, ambapo goli la tano lilisababisha
tweets 580,601 kutumwa katika muda wa dakika moja tu.
Tweets sita kati
ya kumi zilizokuwa zikirindima zaidi zilikuwa zinataja mechi hiyo, huku #BrazilvsGermany
ikirindima zaidi. Miroslav Klose (kwenye picha) ndio alikuwa mchezaji
aliyetajwa zaidi katika twitter, akifuatiwa na Toni Kroos.
Julio Cesar,
Oscar na Fred ndio wachezaji wa Brazil waliotajwa zaidi. Rekodi ya
zamani ya shughuli ya kimichezo ilikuwa katika mechi kati ya Brazil na
Chile, ambapo tweets 389,000 zilitumwa katika kipindi cha dakika moja.
0 comments:
Post a Comment