Facebook

Friday, 11 July 2014

Utandawazi wazidi kushika kasi...Wataalam wagundua miwani inayoweza kusoma mawazo ya mtu.

 Salim Kikeke's photo.

Miwani ya kisasa ya Google imedukuliwa, ambapo sasa inaweza kufanya kazi kwa kusoma mawazo ya mtu.
Mtumiaji anaweza kupiga picha kwa kufikiria tu.

Kwa kutumia miwani hiyo ya kisasa na kuunganisha kichwani na kifaa kijulikanacho kama electroencephalography (EEG) ambapo kifaa uroro huweza kusoma unachofikiria, na hata kupiga picha bila kujigusa au kubonyeza mahala popote.

Salim Kikeke's photo. 
Kampuni ya This Place ya London iliyotengeneza kifaa uroro hicho (software) imesema inaweza kutumika pale watu wanapohitaji kufanya mambo mengine bila kutumia mikono yao, mathalan wakati madaktari wanafanya upasuaji.
This Place imetoa kifaa uroro hicho MindRDR bure na wana imani kuwa huenda wataalam wengine wanaweza kutumia kwa shughuli nyingine.

Salim Kikeke's photo. 
 
Hata hivyo Google imesema haitambui kifaa uroro hicho.
"Miwani yetu ya Google haiweza kusoma mawazo ya mtu" msemaji wa Google amesema.
Kutaka kujaribu kifaa uroro hicho kama una miwani ya Google, ingia:hapa

Related Posts:

  • MIFUPA YA DINOSARIA "GODZILLA" YAPATIKANA TANZANIAAina mpya ya dinosaria imetambuliwa kufuatia kupatikana kwa mifupa nchini Tanzania. Mabaki hayo ya dinosaria yaliyopewa jina la - Rukwatitan Bisepultus - yalipatikana katika korongo moja kwenye eneo la Rukwa, kusini magharibi… Read More
  • Matangazo tiba za asili yapigwa marufuku. Matangazo ya tiba za asili yanaelezwa kupotosha uma Baraza la Tiba za Asili na Tiba Mbadala Tanzania limesitisha vibali vya kurusha matangazo ya tiba za asili na mbadala kwenye vyombo vyote vya habari kwa kile kili… Read More
  • Sigara za Kielektroniki hatari kwa Afya yako. Watafiti wa afya kutoka Marekani wameonya matumizi ya sigara za kielektroniki zilizoandaliwa kuwasaidia wavutaji sigara kuacha uvutaji kwamba zinaweza … Read More
  • Nyani awagawia watu pesa India Nyani hawa aina ya Macaque huabudiwa na watu nchini India Nyani mmoja katika jimbo la Himachal Pradesh Kaskazini ya India, amewagawia watu pesa taslimu kutoka mtini. Taarifa zinasema kuwa watu waliokuwa wanajivinja… Read More
  • Apple wazindua bidhaa mpya.Kampuni ya Apple imezindua saa ya kisasa - the Apple Watch - ambayo ni bidhaa yake mpya tangu iPad ya kwanza na tangu kifo cha mmoja wa waasisi wake Steve Jobs. Kifaa hicho huendesha programu tumishi (apps) na pia hufuatilia … Read More

0 comments:

Post a Comment