Serikali ya Brazil inapendekeza
kuwapa nyongeza ya asilimia 15.8 mishahara polisi wake ili wasigome
wakati wa ufunguzi wa michuano ya kombe la dunia wiki ijayo.
Maafisa wakuu wa polisi watapokea nyongeza ya asilimia 12 kuanzia mwezi Julai na nyingine ya asilimia 3.8 mwezi Januari.Maandalizi ya kombe la dunia ambalo linaanza tarehe 12 Juni, yamekumbwa na maandamano ya kupinga serikali kwa kutumia gharama kubwa kuandaa michuano hiyo.
Polisi ambao hukabiliana na vitendo vya uhalifu na kupambana na ulanguzi wa madawa ya kulevya pamoja na ugaidi, pia watahakikisha usalama mipakani na katika viwanja vya ndege.
'Mgomo wasitishwa'
Mkuu wa chama hicho alisema kuwa serikali pia imekubali kubuni kikundi cha waakilishi watakaozungumzia swala la kuwapandishwa vyeo polisi waliofika kiwango hicho.
Mwezi jana polisi hao waligoma wakitaka kuongezwa mishahara katika majimbo 14 nchini humo huku walimu na wafanyakazi wa umma pia wakidai mazingira bora ya kazi na nyongeza ya mishahara.
Serikali imeimarisha usalama katika maeneo yote 12 yatakayotumiwa kwa michuano hiyo huku polisi 20,000 wakitarajiwa kudhbiti ulinzi mjini Rio.
Wadadisi wanasema kuwa hatua ya serikali ni kutaka kuhakikisha kuwa maandamano yaliyoshuhudiwa wakati wa kombe la mashirikisho mwaka jana hayatashuhudiwa tena.
Tuko katika maboresho hivi karibuni
blog hii itakuwa ni site ambayo itaitwa www.bantutz.com ni katika hatua za kuboresha huduma zetu za
kutoa habari,tutakuja katika muonekano mpya na bora zaidi.
0 comments:
Post a Comment