Facebook

Monday, 14 July 2014

Vita kati ya Israel na Palestina vyazidi kupamba moto.

 Photo: Israel na wapiganaji katika Gaza wameendelea kurushiana makombora usiku kucha baada ya Israel kuahidi kuendelea na mashambulizi ili kuzuia maroketi.
Wapalestina wapatao 121 wameuawa, kwa mujibu wa vyanzo vya Palestina. Umoja wa Mataifa umesema robo tatu ya waliouawa ni raia.
Israel imesema imeshambulia "vituo 60 vya magaidi" katika mashambulio mapya. Maroketi mawili yamegonga mji wa Beersheba, limesema jeshi la Israel. 
Mamia ya makombora na maroketi yamevurumishwa tangu Israel ilipoanza harakati zake siku tano zilizopita.
Israel inasema inalenga wanamgambo na vituo vyao, ikiwa ni pamoja na makazi ya viongozi wa wapiganaji. Inasema "magaidi kadhaa" ni miongoni mwa waliouawa.
Waziri mkuu Wa Israel Benjamin Netanyahu alisema siku ya Ijumaa kuwa nchi yake haitatikiswa na shinikizo la kimataifa kusimamisha harakati zake.
Israel na wapiganaji katika Gaza wameendelea kurushiana makombora usiku kucha baada ya Israel kuahidi kuendelea na mashambulizi ili kuzuia maroketi.
Wapalestina wapatao 121 wameuawa, kwa mujibu wa vyanzo vya Palestina. Umoja wa Mataifa umesema robo tatu ya waliouawa ni raia.
Israel imesema imeshambulia "vituo 60 vya magaidi" katika mashambulio mapya. Maroketi mawili yamegonga mji wa Beersheba, limesema jeshi la Israel.
Mamia ya makombora na maroketi yamevurumishwa tangu Israel ilipoanza harakati zake siku tano zilizopita.
Israel inasema inalenga wanamgambo na vituo vyao, ikiwa ni pamoja na makazi ya viongozi wa wapiganaji. Inasema "magaidi kadhaa" ni miongoni mwa waliouawa.
Waziri mkuu Wa Israel Benjamin Netanyahu alisema siku ya Ijumaa kuwa nchi yake haitatikiswa na shinikizo la kimataifa kusimamisha harakati zake.

0 comments:

Post a Comment