Facebook

Tuesday, 8 July 2014

Ebola yaanza kuonekana Ghana.

 Photo: EBOLA YAONEKANA GHANA
Ghana inatibu mtu mmoja anayedhaniwa kuwa na Ebola, kwa mujibu wa wizara ya afya.
Ebola imesababisha vifo vya zaidi ya watu 460 mpaka sasa tangu ugonjwa huo ulipoanza nchini Guinea mwezi Februari, na kusambaa katika nchi jirani za Liberia na Sierra Leone.
Ugonjwa huo hauna chanjo wala tiba.
Wizara ya afya imesema imeweka "hatua za tahadhari" na kuwa watu wawe watulivu.
Mtu huyo anatibiwa katika zahanati ya Nyaho, mjini Accra, imesema wizara ya afya katika taarifa yake.
Mgonjwa huyo pamoja na wafanyakazi wa zahanati wamewekwa chini ya karantini na kupatiwa vifaa vinavyotakiwa, imesema taarifa hiyo.

Related Posts:

0 comments:

Post a Comment