Watu wasiopungua 20 wameuawa katika mashambulio mawili katika kaunti mbili kwenye pwani ya Kenya usiku wa kuamkia Jumapili.
Watu walioshuhudia matukio hayo wamesema, watu wenye silaha nzito walishambulia eneo la biashara katika kijiji cha Hindi, kaunti ya Lamu, na pia kituo cha polisi cha Gamba, katika kaunti ya Tana River.
Katika kijiji cha Hindi, polisi walikuta miili 11 imetapakaa katika mashamba. Daily Nation imeripoti kuwa watu 10 na mtoto mmoja wa kiume wameuawa katika shambulio la Hindi, eneo la Malamandi.
Katika shambulio jingine, watu wenye silaha wameshaambulia kituo cha polisi na kuua watu tisa papo hapo, akiwemo afisa wa polisi aliyekuwa zamu. Washambuliaji hao wanadaiwa pia kumwachilia huru mmoja wa washukiwa wa tukio la Mpeketoni, aliyekuwa akishikiliwa hapo.
Kundi la al-Shabab limedai kuhusika na mashambulio hayo.
Gazeti la Nation la Kenya limeripoti kuwa Naibu Rais William Ruto aliyekuwa afanye ziara katika mji wa Mpeketoni, ameahirisha ziara hiyo.
0 comments:
Post a Comment