Facebook

Thursday, 3 July 2014

Hazard akataa kulinganishwa na Messi

Eden Hazard amesema ana nia ya kufikia kiwango cha Lionel Messi, ila kwa sasa sio lengo lake.
Eden Hazard amesema ana nia ya kufikia kiwango cha Lionel Messi, ila kwa sasa sio lengo lake.
Eden Hazard amekataa kulinganishwa kwa ubora na mshambuliaji hatari wa Argentina Lionel Messi, wachezaji hao wawili  watakutana siku ya Jumamosi kwenye mechi kali inayotarajia kuvuta hisia za wengi ambapo Ubelgiji wataumana na Argentina.
Hazard alikuwepo kwenye kikosi kilichoiangamiza Marekani magoli 2-1 mara baada ya timu hizo kucheza dakika 120 katika mechi ya Kombe laDunia iliyofanyika Jijini Salvador siku ya Jumanne.
Katika mechi ya robo fainali Ubelgiji itakutana na Argentina iliyoifungashia virago Uswizi kwa goli alilofunga winga wao Angel Di Maria.
Katika kujianda na mechi hiyo ya mwishoni mwa juma viwanja vya mazoezi vya timu hizi mbili katika nyakati tofauti pamoja makocha wao wanatarajia kuugusia vita kali ya kwenye nyasi kati ya winga wa Chelsea Hazard na mshambuliaji wa Barcelona Messi.
Hata hivyo Hazard amesisitiza bado yupo njiani katika safari yake ya kufikia kiwango alichonacho mshambuliaji huyo wa Argentina mwenye tuzo nne za mchezaji bora wa Dunia wa Fifa.
”Nina wakubali wachezaji kama Messi. Leo mimi sipo katika ubora waliopo. Bado ni nao muda wa kuwafikia ingawaje hilo sio lengo langu kwasasa. Lengo langu ni hatua ya mtoano.”
“Argentina hawana Messi peke yake. Wana wachezaji wazuri lakini wanamtegemea sana Messi. Anaweza kubadilisha matokeo katika wakati wowote”, alieleza Hazard.
Hazard anahisi Ubelgiji wanayo kila sababu ya kusonga mbele katika michuano ya Kombe la Dunia na wangefanya hivyo ndani ya dakika 90 kama sio uhodari wa mlinda mlango wa timu ya taifa ya Marekani Tim Howard aliyeokoa  michomo ya wazi 15 na kuvunja rekodi iliyowekwa kwenye michuano ya Kombe la Dunia iliyo fanyika mwaka 1966.
”Howard alikuwa hodari katika mchezo huu na kama sio yeye tungekuwa tumeshaibuka na ushindi mapema.
“Tulikua na wasiwasi pale walipo badili matokeo nakuwa 2-1. Tulikua tumechoka lakini tulijikaza na mlinda mlango wetu Thibaut Courtois akatuokoa.”
“Tulicheza mchezo mzuri, na tulijitolea kwa kujituma kwa kila hali, na kwaushirikiano”, aliongeza
Inasemekana siku hiyo ya Jumamosi mtoto hatotumwa dukani.

Related Posts:

0 comments:

Post a Comment