
Uwanja wa ndege wa kimataifa wa Libya umeshambuliwa na mabomu, siku moja baada ya mapigano kulazimisha uwanja huo kufungwa.
Picha zimeonesha ndege kubwa ya abiria ikiwaka moto ripoti zikisema baada ya kupigwa na roketi kwenye uwanja huo wa Tripoli siku ya Jumatatu. Watu wasiopungua saba waliuawa karibu na uwanja huo siku ya Jumapili.
Umoja wa Mataifa umetangaza kuwa utaondoa wafanyakazi wake wote kutoka Libya.
Viongozi wa Libya wamekuwa wakipata tabu kuleta hali ya utulivu nchini humo tangu Muammar Gaddafi kuondolewa madarakani mwaka 2011.
Vyanzo vya habari vya kiusalama vimesema kuwa uwanja huo ulishambuliwa na "idadi kubwa ya maroketi, yakiwemo maroketi ya Grad" siku ya Jumatatu.
Hakuna taarifa za vifo au majeruhi katika shambulio la Jumatatu, lakini ndege moja inadhaniwa kuteketezwa.
Ndege zote zinazopaa na kutua zimesitishwa hadi pengine siku ya Jumatano.
0 comments:
Post a Comment