Bunge la Burundi limepitisha muswada unaolenga kupambana na "mfumuko wa makanisa" nchini humo.
Utafiti wa serikali mwaka jana uligundua kuwepo na madhehebu 557. Sheria mpya zinataka makanisa kuwa na wafuasi wasiopungua 500 na jengo rasmi.
Makanisa ya kiinjili yaliibuka wakati, na baada ya vita vya muda mrefu vya wenyewe kwa wenyewe vilivyomalizika mwaka 2005.
Mwandishi mmoja anasema muswada huo umepita bila kupingwa katika bunge na hauna dalili za kupingwa katika bunge la seneti. Iwapo hakuna mabadiliko yatafanywa katika muswada huo, lazima utiwe saini na rais ndani ya siku 30, au kurejeshwa tena kwa wabunge ili kutazamwa tena. Mara baada ya muswada huo kufanywa kuwa sheria, makanisa yatakuwa na mwaka mmoja kuanza kufuata sheria hiyo.
Ni jambo la kawaida kuona mahema yakigeuzwa kuwa makanisa pembezoni mwa barabara,

0 comments:
Post a Comment