Tayari tumeona bondia Mayweather akitoa
ushahidi wake kufuatia ugomvi mkubwa ulioibuka kati yake ya Rapa T.I juu
ya usaliti na mke wake Tameka au Tiny na kusema Tiny ndie
aliyesababisha kila kitu ambapo wapenzi hao hawakujibu chochote lakini
sasa wameamua kuvunja ukimya kila mtu kwa wakati wake.
Kupitia Instagram, Tiny alianza kwa
kuwashukuru mashabiki wake waliosimama pamoja nae na kuwaponda waliokuwa
wakimsema lakini akafunguka kuwa mara nyingi mpenzi wake amekuwa
akionekana na wasichana wengine lakini yeye alinyamaza tu hakusema
chochote iweje watu wahoji baada ya yeye kuonekana na Mayweather?
Baada ya kukaa kimya kwa muda, Rapa T.I nae akaamua kujibu kupitia Instagram kuwa alijua ishu nzima baada ya kuambiwa kila kitu na kusema hajali tena lakini pia alionyesha kupitia video mkono wake akiashiria kwamba kweli aliingia katika ugomvi na mtu
Endelea kutembelea katemimethsela.blogspot.com kupata stori mbalimbali zinazohusiana na mastaa
0 comments:
Post a Comment