Wakuu katika shrika la kupambana na rushwa nchini Nigeria
wanasema maafisa kadhaa kutoka benki kuu ya nchi hiyo
wamepelekwa mahakamani kwa tuhuma za ufisadi wa kiasi kikubwa
cha fedha za thamani ya mamilioni ya dola.
Pia baadhi ya maafisa wa benki za kibiashara wamo kwenye orodha
hiyo ya watuhumiwa baada ya kushukiwa kuhusika kwenye
udanganyifu mkubwa wa pesa.
Shirika hilo la kupambana na ufisadi The Economic and Financial
Crimes Commission lilimeuelezea udanganyifu huo wa fedha kuwa
walijaribu kuingiza katika soko la fedha noti ambazo zilikuwa tayari
zimeondolewa kutoka soko hilo na zilitakiwa kuharibiwa kabisa kwa
kuwa zimezeeka au kwa sababu nyengine yeyote.
Katika ulaghai huo wahusika wanasemekana walitengeneza vipande
vya magazeti kwa kiwango na ukubwa sawa na hizo noti za
kuharibiwa na kudanganya kuwa wanachoma noti hizo zilizopigwa
marufuku na badala yake kuzirudisha kwa matumizi ya kila siku ya
kifedha hivyo kujipatia faida kubwa ya fedha halisi.
Waliokamatwa ni maafisa 6 wa benki kuu ya Nigeria wanaofanya kazi
mjini Ibadan na wafanyikazi 16 kutoka benki za kibinafsi ambao pia
wanatuhumiwa kushiriki kashfa hiyo.
Nigeria
Ufisadi na Udanganyifu huo umeipa hasara Nigeria ya zaidi ya dolla
million 30.
Ingawaje kamata kamata hiyo ilifanyika kabla ya kuapishwa kwa
rais mpya wa Nigeria, Muhammadu Buhari, wengi wanamuona kama
ndiye kichochezi kikubwa kilichosababisha hatua hiyo kutokana na
msimamo wake mkali wa kupambana na rushwa nchini humo.
Kwa miaka mingi vita dhidi ya ufisadi nchini humo vimewalenga zaidi
walarushwa wadogo huku wala rushwa wakubwa wakikwepa mkono wa
kisheria kwa kutumia hizo hizo fedha walizozipata kwa njia za
kifisadi.
Monday, 1 June 2015
Benki Kuu Nigeria yakumbwa na kashfa ya Ufisadi.
Related Posts:
Daktari wa Ebola apata maambukizi Sierra Leone. Daktari anayeongoza vita dhidi ya ugonjwa wa Ebola nchini Sierra Leone ameambukizwa virusi hivyo na sasa anatibiwa, imesema taarifa kutoka ikulu. Vipimo kwa Sheik Umar Khan vilionesha ana virusi hivyo na amelazwa k… Read More
Shambulio katika kikosi cha Kumlinda Rais wa DRC lashundikana. Shambulio katika kambi ya jeshi ya kikosi cha kumlinda rais wa Jamhuri ya Kidemokrasi ya Kongo limezuiwa, kwa mujibu wa maafisa wa serikali. Hali imerejea kuwa ya utulivu na kundi dogo la "waliojipenyeza" limezid… Read More
Mbunge na Mwanamuziki maarufu Somalia apigwa risasi na kufariki. Mwanamuziki maarufu ambaye pia ni Mbunge nchini Somalia, Saado Ali Warsame amepigwa risasi na kufa na wanamgambo. Aliuawa pamoja na mlinzi wake, katika shambulio la kutumia gari mjini Mogadishu. Msemaji wa kundi … Read More
Ndege nyingine yadondoka yaua zaidi ya watu 40 Taiwan. Ndege ya Abiria ya Kampuni ya Trans Asia ya Taiwan imedondoka wakati ikijaribu kutua kwa dharura na kusababisha vifo vya watu zaidi ya 40… Read More
Wapalestina wengi wazidi kuawa Gaza Mmoja kati ya majeruhi wa mapigano eneo la Gaza Kumetokea vifo vingi katika eneo la Gaza kwa siku moja tangu kuanza kwa mashambulizi ya Israel dhidi ya Palestina mapema mwezi huu. Wapalestina zaidi ya sitini kati y… Read More
0 comments:
Post a Comment