Facebook

Friday, 18 July 2014

Tetesi za Usajili katika magazeti mbalimbali barani Ulaya.


Salim Kikeke's photo. 
Chelsea wapo tayari kumuuza John Obi Mikel, 27, wakati wanapanga kumnyatia kiungo wa Real Madird Sami Khedira, 27 ambaye pia anatakiwa na Arsenal (Daily Express), 
 Salim Kikeke's photo.
Arsenal wanatarajia kuthibitisha siku ya Alhamisi usajili wa kiungo wa Newcastle Mathieu Debuchy, 28, kwa pauni milioni 10 (London Evening Standard), 

Tottenham watampa beki Jan Vertonghen, 27, mkataba mpya wa miaka mitano, pamoja na kuongeza mshahara hadi pauni 45,000 kwa wiki (Daily Mail),
 Salim Kikeke's photo.
Kocha mpya wa Manchester United Louis van Gaal anataka kuwaondoa takriban wachezaji kumi wakiwemo Ashley Young, Patrice Evra, Fellaini, Nick Powell, Anderson, Javier Hernandez, Wilfried Zaha, Nani, Tom Cleverly, Chris Smalling na Bebe (Daily Star na Daily Mirror), 

Mark Hughes wa Stoke City yuko karibu kumchukua winga wa Liverpool Oussama Assaidi, 25 kwa uhamisho wa takriban pauni milioni 7 (Daily Telegraph), 

Meneja wa QPR Harry Redknapp anapanga kumchukua beki wa kati wa Aston Villa Ron Vlaar kwa pauni milioni 4 (Birmingham Mail),

Liverpool watapambana na Tottenham kumwania beki wa kushoto wa Swansea Ben Davies (Daily Star),

 Toni Kroos anajiandaa kuhamia Real Madrid kwa mkataba wa euro milioni 30 akitokea Bayern Munich (Bild). Tetesi nyingine kesho tukijaaliwa.

Related Posts:

  • Tetesi zote za Usajili wa wachezaji barani Ulaya siku ya leo.Dau la Manchester United la pauni milioni 110 kwa Real Madrid kumtaka Gareth Bale, 25 na beki Rafael Varane, 22 limekataliwa na klabu hiyo ya La Liga (Daily Express),   Real Madrid wana uhakika wa kumsajili kwa pauni m… Read More
  • Singano "Messi" katika mtihani mzito Msimbazi. SIMBA SC inajipanga kumchukulia hatua mchezaji wake, Ramadhani Singano ‘Messi’ kwa kuituhumu klabu hiyo kughushi Mkataba wake. Mkuu wa Idara ya Habari na Mawasiliano ya Simba SC, Hajji Sunday Manara ‘Zungu’ amefanya Mkut… Read More
  • Chelsea yarusha ndoano kwa Gundogan.Timu ya chelsea inatajwa katika mbio za kuhitaji saini ya mchezaji IIkay Gundogan kutoka Dortmund lakini taarifa zinasema mchezaji huyo yupo katika mazungumzo na vilabu vingine vya Barcelona, Manchester United.Bayern na Ars… Read More
  • Mbeya City yafungua ukurasa wa usajili.Mshambuliaji wa kutumainiwa wa Ndanda Fc, Gideon Benson amesaini kandarasi ya mwaka mmoja na nusu kujiunga na kikosi ch Mbeya City fc kinachonolewa na Juma Mwambusi katika msimu ujao Benson ameweka kando ofa kadhaa aliz… Read More
  • Man City yamnyatia Isco.Manchester City inataka kupata saini ya kiungo wa Real Madrid Isco. Mchezaji huyo miaka 23 hajui hatima yake Santiago Bernabeu baada ya ujio wa meneja mpya Rafa Benitez.Isco alijiunga na Real Madrid kwa ada ya Euro milioni30 … Read More

0 comments:

Post a Comment