Wachezaji saba wa Ujerumani wana dalili za ugonjwa wa mafua, saa 24 kabla ya mechi yao ya Kombe la Dunia dhidi ya Ufaransa.
Kocha wa Ujerumani Joachim Low amesema wengi wao wana "maumivu ya koo" lakini hakutaja majina ya wachezaji hao.
"Ni mapema mno kufanya mabadiliko yoyote kwenye kikosi kitakachoanza" amesema Low.
Kocha wa Ujerumani Joachim Low amesema wengi wao wana "maumivu ya koo" lakini hakutaja majina ya wachezaji hao.
"Ni mapema mno kufanya mabadiliko yoyote kwenye kikosi kitakachoanza" amesema Low.
Mat Hummels na Christoph Kramer waliugua mapema wiki hii,
Hummels akikosa mchezo dhidi ya Algeria. Low anaamini kuwa safari kutoka
mji mmoja kwenda mwingine nchini Brazil, hali ya hewa na mvua pamoja na
baridi mjini Porto Alegre huenda zimechangia.
Lakini ameongeza kuwa
"Hali si mbaya sana kwa sasa. Sitaki kulifanya jambo hili kuwa kubwa."
0 comments:
Post a Comment