Facebook

Monday, 7 July 2014

Van Gaal aeleza sababu za kubadili kipa.

 Photo: VAN GAAL AELEZA SABABU ZA KUBADILI KIPA
Kocha wa Uholanzi Luis van Gaal amesema urefu wa kipa Tim Krul ndio ulimfanya amchezeshe katika mikwaju ya penati katika mchezo wa robo fainali dhidi ya Costa Rica.
Krul, mwenye urefu wa futi 6 na inchi 4, (mita 1 sentimita 93) aliingia badala ya kipa aliyeanza Jasper Cillessen zikiwa zimesalia sekunde chache kabla ya mikwaju ya penati kuanza kupigwa. Jasper ana urefu wa futi 6 inchi 2 (Mita1 sentimia 87).
Krul aliweza kupangua penati mbili, na hivyo Uholanzi kushinda kwa magoli 4-3.
"Tulidhani kuwa TIm ndio kipa bora wa kuzuia penati," alisema Van Gaal. "Ni mrefu na ana nafasi zaidi ya kuzuia."
Menenja huyo wa Manchester United aliongeza kusema: "Ilifanikiwa, ilienda vyema. Ninajivunia kidogo kwa hilo."
Uholanzi, timu pekee kati ya nne zilizosalia ambayo haijawahi kushinda Kombe la Dunia, itapambana na Argentina mjini Sao Paulo siku ya Jumatano. Brazil itacheza na Ujerumani katika nusu fainali ya kwanza siku ya Jumanne.

Related Posts:

  • Hazard akataa kulinganishwa na Messi Eden Hazard amesema ana nia ya kufikia kiwango cha Lionel Messi, ila kwa sasa sio lengo lake. Eden Hazard amekataa kulinganishwa kwa ubora na mshambuliaji hatari wa Argentina Lionel Messi, wachezaji hao waw… Read More
  • Timu ya taifa ya Rugby ya Kenya yajihakikishia kufuzu.     Timu ya taifa ya Rugby ya Kenya imeichapa Madagascar 34-0 katika mchezo wa kufuzu kucheza Kombe la Dunia England 2015. Hata hivyo wanahitaji kushinda mchezo dhidi ya Zimbabwe siku ya Jumapili kujihakikis… Read More
  • FIFA yampa ruksa Suarez kufanya mazoezi   FIFA imesema Luis Suarez ataruhusiwa kufanya mazoezi na Liverpool wakati akitumikia adhabu yake ya miezi minne na mechi nane za kimataifa. Wakati huohuo Uruguay imekata rufaa kupinga adhabu hiyo. Suarez ali… Read More
  • Wachezaji saba wa Ujerumani waugua mafua.     Wachezaji saba wa Ujerumani wana dalili za ugonjwa wa mafua, saa 24 kabla ya mechi yao ya Kombe la Dunia dhidi ya Ufaransa. Kocha wa Ujerumani Joachim Low amesema wengi wao wana "maumivu ya koo" lakini ha… Read More
  • Neymar azungumzia kuhusu "Pressure" walionayo.     Neymar amekuwa akigonga vichwa vya habari katika magazeti ya Brazil asubuhi ya leo. Namba 10 huyo wa Brazil akizungumza na waandishi wa habari jana, na alipoulizwa kuhusu 'uzito' alionao mabegani kuto… Read More

0 comments:

Post a Comment