Facebook

Wednesday, 9 July 2014

Watu 50 wakamatwa wanaoshukiwa katika milipuko Kenya.

 Photo: 50 WAKAMATWA KENYA 
Naibu Rais wa Kenya Wiliam Ruto amesema washukiwa 50 wamekamatwa kuhusiana na machafuko yaliyotokea siku chache zilizopita katika eneo la pwani ya Kenya. Serikali imeahidi kuwasaka wote waliohusika na mashambulio katika vijiji na miji iliyopo karibu na kisiwa cha Lamu. Mamia ya watu wamekimbia makazi yao katika eneo hilo. Wakazi wa huko pia wamesema wamekuta vijikaratasi vinavyotishia Wakristo. Vijikaratasi hivyo vinadaiwa kutoka kwa kundi la al-Shabab. Kundi hilo limekanusha kuhusika na vijikaratsi hivyo.

Related Posts:

0 comments:

Post a Comment