Facebook

Tuesday, 1 July 2014

DIEGO COSTA:KUMBE NDIVYO ILIVYO??


Ukistaajabu ya Musa utayaona ya
Firauni,msemo huu hutumika sana
kunapotokea jambo lisilo la kawaida.
Hivi unafahamu yaliyojificha nyuma ya usajili
wa mshambulizi Diego Costa kuelekea klabu ya
Chelsea?


Acha nikupe mchapo na ishu iko hivi baada ya
klabu ya Chelsea kuonyesha nia ya kumtaka
Diego Costa wakala wake muhuni mmoja hivi
aitwae Jorge Mendez akaona yessss ulaji
huoooooo umejileta.
Kama kawaida yake bwana Jorge Mendez
ukipenda muite mzee wa magumashi baada ya
kufanya mazungumzo na Chelsea akachekecha
akili weeeeeeee akaona isiwe tabu
akamwambia Diego mwanangu nataka uende
darajani ila kabla ya yote kwanza tuwekeane
mkataba.
Napambana uondoke Vicente Cardeloni lakini
ikiwa usajili huu ukishindwa kufanikiwa na
sababu ukiwa ni wewe mwanangu lazima
unilipe mamilioni ya Euro.
Mendez kama kawaida yake akachukua kitu
cha fast jet huyooooooo mpaka London hapa
yeye hapa Mourinho mambo yakajipa.Diego
akasubiri mara majeruhi mara Uefa heeeh
ghafla tamaa ya kubaki Atletico Madrid
ikamuingia,Mendez akamwambia weeeee
kumbuka makubaliano ya ule mkataba Diego
akaishiwa pozi.Kubaki kuna mtaka kuondoka
kuna muita akabaki njia panda haendi wala
harudi.
Mendez akawaambia Chelsea kazi ndogo tuu
cha kufanya chukua washikaji zake chukua
Felipe Luiz chukua Tiago ,Diego mtamng'oa
tuu hana ujanja ukiwa na watu hapo darajani
atatulia kama maji mtungini.
Kwakuwa Chelsea ni watu wa umate umate
wakaona isiwe tabu �33m za Diego hizi hapa
�20m za Felipe hizi hapa mchezo ukawa
umeisha hivi ninavyokwambia utasikia ya
kusikia wee kaa mkao wa kula.
Hivi we umeshajiuliza Tiago na miaka yake 33
anakwenda Chelsea kufanya nini?kucheza?Ahh
wapi yule ni chambo tuu mpango mzima uko
kama nilivyokutonya.

0 comments:

Post a Comment