KLABU ya Ureno Sporting Lisbon imethibitisha
kuwa wao na Manchester United wamekubaliana
Uhamisho wa Beki kutoka Argentina Marcos Rojo
kwenda Man United na Nani kutua huko Lisbon
kwa Mkopo wa Msimu mmoja.
Sporting Lisbon wao ndio walikuwa wa kwanza
kuanika habari hizi kwa njia ya Mtandao wa
Twitter wakithibitisha Rojo kwenda Old Trafford
na Nani, Winga wa Man United aliehamia hapo
kutoka Sporting Lisbon Mwaka 2007, kurudi
kwao kwa Mkopo wa Mwaka mmoja.
Hivi punde, Klabu ya Man United imethibitisha
Dili hii na kusema itakamilika baada ya upimwaji
afya Rojo na makubaliano ya maslahi binafsi.
Awali Rojo alithibitisha kuhamia Man United hata
kabla habari hizi kutolewa na Sporting Lisbon na
pia kusema anatarajia Leo hii kusafiri kwenda
Jijini Manchester.
Mapema Rojo alikaririwa kusema: “Ni kama
ndoto kuwa Mchezaji wa Manchester United!
Kuhama Sporting haikuwa rahisi!”
Hivi sasa pia zimeibuka ripoti kuwa Rojo
aliisapoti Picha yake na Di Maria iliyowekwa
kwenye Mtandao wa Instagram wakikumbatiana
mbele ya Nembo ya Man United ikiwa ni ishara
ya wazi kuwa wawili hao wako njiani kutua Old
Trafford.
Rojo alihamia Sportung Lisbon Mwaka 2012
akitokea Spartak Moscow na Kampuni ya Doyen
Sport ililipa Asilimia 75 na Sporting Lisbon kulipa
Asilimia 25 ya Ada ya Uhamisho wake.
Rojo alicheza Mechi zote za Argentina huko
Brazil kwenye Fainali za Kombe la Dunia ambapo
Argentina ilifungwa kwenye Fainali Bao 1-0 na
Germany na Meneja wa Man United, Louis van
Gaal, anamwona Beki huyo ni kiraka kwenye
Mfumo wake wa 3-5-2 kutokana na uwezo wake
wa kucheza Sentahafu au Fulbeki wa Kushoto.
Beki huyo yumo kwenye Timu ya FIFA ya Fainali
za Kombe la Dunia za Brazil 2014.
Kabla kuhamia Spartak Moscow na kisha Sporting
Lisbon, Rojo aliichezea Estudiantes ya Argentina
na kutwaa Copa Libertadores Mwaka 2009.
Tuesday, 19 August 2014
Rojo atua rasmi Manchester United,Nani aenda Sporting Lisbon kwa mkopo.
Related Posts:
Angel Di Maria "Nabaki old TraffordMchezaji raia wa Argentina Angel di Maria amethibitisha kubaki Manchester United msimu ujao. Pamoja na tetesi za kujiunga PSG kwa ada ya ya Euro milioni 60. Di Maria amefunga magoli manne na kutoa pasi za magoli 12 kwa mash… Read More
Hawa ndio wachezaji waliochaguliwa katika timu bora ya wiki hii katika michuano ya Ligi ya Mabingwa barani Ulaya.Hawa ndio wachezaji waliochaguliwa katika timu bora ya wiki katika michuano ya Ligi ya Mabingwa barani Ulaya. 1.Gianluigi Buffon 2.Alessandro Florenzi 3.Diego Godin 4.Kostas Manolas 5.Angel Di Maria 6.Thiago Alcantara 7.Hakan… Read More
Chicharito ameanza kufunga Bayern Leverkusen.Mchezaji wa zamani wa United, Javier Hernandez amefunga goli lake la kwanza kwa Bayer Leverkusen ya Ujerumani katika mchezo wa Champions League wa ushindi wa magoli 4 - 1 nyumbani dhidi ya ATE Borisov. … Read More
Mourinho "Nilisahau utamu wa ushindi"Kocha mkuu wa Chelsea Jose Mourinho amesema alikuwa amesahau utamu wa ushindi akizungumza baada ya vijana wake kujikwamua na kupata ushindi wa 4-0 dhidi ya Maccabi Tel Aviv. Hii ni baada ya klabu hiyo kuanza vibaya ligi ya Pr… Read More
Henderson afurahia Brendan Rodgers kubaki Liverpool.Kiungo Jordan Henderson amefurahia maamuzi ya uongozi kumbakisha kocha wa Liverpool Brendan Rodgers Kapteni huyo amesisitiza watamaliza msimu ujao kwa mafanikio na kuiletea heshima timu hiyo. Kocha Rodgers alikuwa na wakati m… Read More
0 comments:
Post a Comment