Facebook

Saturday 11 April 2015

Angelo Henriquez:Nimatarajio yangu kurejea Manchester United

A user's photo.

Angelo Henriquez yupo wazi katika uwezekano wa yeye kurejea katika klabu yake ya Manchester United katika siku za mbeleni lakini amekiri kua alikatishwa tamaa najinsi maisha yake ya kisoka yalivyo kwenda katika klabu hiyo.
akiwa amefurahia mafanikio katika kombe la FA akiwa na klabu ya Wigan kwa mkopo,Henriquez alipata uzoefu wakutosha lakini sicho alicho kitarajia.
Mchezji huyo mwenye umri wa miaka 20 kwa sasa amekua katika timu ya Dinamo Zagreb kwa mkopo wa mwaka mmoja na amweza kufanya vyema kwa kufunga magoli ya kutosha.
Huku klabu hiyo toka nchini Croatia ikiwa na chaguo la kumnunua katika makubaliano yao ya mkopo,walikuwa wanatarajia kumsajili mchezaji huyo raia wa nchini Chile lakini Henriquez ameongea juu ya yeye kutaka kurejea katika maisha yake yasoka akiwa na klabu yake ya Manchester United
"natarajia kurejea Manchester United siku za mbeleni,nilishangazwa kwa sababu nilikua bado kidogo tu nianze kucheza katika kikosi cha kwanza na nilitakiwa nitafute nafasi hiyo toka kwa timu nyingine.jambo hilo lilini koroga"
"nilikuja na matarajio ya kucheza ligi kuu ya England na kombe la FA lakini hakuna kilicho tokea.nilicheza katika mechi za vijana wachini ya umri wa miaka 21 pekee"
mapema mwaka huu ,Henriquez alisema alikuwa anatarajia kuwa katika timu ya Dinamo kwa muda mrefu lakini kwa sasa raia huyo wa Chile amesisitiza anataka kurudi Manchester United.
kwa sasa mambo yapo hewani,haijulikani kama Henriquez atajifunga kuitumikia klabu hiyo kwa moja kwa moja au Van Gaal ata chagua muda sahihi kama akitakiwa kuondoka klabuni hapo.

0 comments:

Post a Comment