Facebook

Tuesday 14 April 2015

UCHAMBUZI WA MECHI ZA LEO ROBO FAINALI LIGI YA MABINGWA BARANI ULAYA-UEFA.

ATLETICO MADRID vs R.MADRID:-VICENTE CALDERON 21:45
         Walicheza fainali ya UEFA msimu uliopita kukutana tena katika hatua ya robo fainal msimu huu wa Uefa,kama unakumbuka  tulishuhudia Real Madrid wakitawazwa mabigwa wa Uefa baada ya kuibuka na ushindi wa goli 4-1 dhidi ya majirani zao Atletico Madrid

    Baada ya fainal hiyo na kipigo hicho kwa vijana wa Simeone Real wamekuwa na wakati mgumu sana pindi wakikuta na A.madrid kwani katika michezo sita wameshindwa kuibuka na ushindi huku kipigo kikubwa walicho kipata kikiwa ni 4-0 pale Vicente Carderon.

     Atletico Madrid wapo nafasi ya 3 katika msimamo wa La-Liga huku Real wakiwa nafasi ya 2 na ukitizama viwango vyao katika Ligi Real Madrid wanafanya vyema zaidi ya Atletico Madrid na kwa namna moja mabingwa watetezi wa La-Liga Atletico Madrid wana nafasi finyu sana kutetea ubingwa wao.

    Licha ya viwango vyao katika ligi ,utofauti wa nafasi walizopo pindi timu hizi zikikutana historia huwa haina nafasi imekuwa ni moja ya michezo migumu kutabiri matokeo kutokana na kukamiana kwao.
    Vikosi havita kuwa na mabadiliko kwa upande wa Atletico Madrid, Raul Garcia ndo anaweza kukosekana na upande wa Real, Fabio Coentrao hatokuwemo.
     Umakini hasa utahitajika ktk safu za ulinzi kwa timu zote kutokana na viwango bora vya washambuliaji kwa upande wa Real C.ronaldo na A.madrid ni Mfaransa Griezmann.
     Sio mchezo wa kukosa ambao pia tutaraji kadi nyingi zikitolewa na vita vikali ktk safu ya kiungo.

JUVENTUS vs MONACO :-JUVENTUS STADIUM
   Kibibi kizee cha Turin watacheza dhidi ya Monaco ya Ufaransa na kutukumbushia nusu fainal ya 1998 ambapo hat-trick ya Mfalme Del Piero na goli la Zidane liliwapa Juve ushindi wa goli 4-1 kwa upande wa Monaco Costinha ndo alikuwa mfungaji.

     Juventus baada ya matokeo mazuri takribani michezo 26 huku wakiwa vinara wa Serie A kwa tofauti ya pointi 12 na Lazio wikendi hii walipoteza dhidi ya Parma mchezo ambao wengi hawakutaraji kama Parma itakuwa kizuizi kwa Juve.
     Huenda Pirlo akarejea ktk mchezo huu kuimarisha safu ya kiungo ambayo imekuwa na kiwango bora kabisa pamoja na safu ya ushambuliaji inayo ongozwa na Tevez mtu ambaye safu ya ulinzi ya Monaco wasipo kuwa nae makini yatawakuta kama yalivyo wakuta Dortmund.
     Kikosi cha  Leonardo Jardims hakina takwimu za matokeo mazuri ktk ligi kuu ya Ufaransa, licha ya kuitoa Arsenal na kufudhu robo fainal bado kumekuwa na umakini mbovu ktk safu ya ulinzi hasa namba 4-5 ambao wamekuwa wakifanya makosa ya mara kwa mara kitu ambacho kinaweza ondoa ndoto zao za kucheza fainal kama ilivyo kuwa 2004 wasipo jirekebisha dhidi ya Juventus.
   Mashambulizi ya kushtukiza yatakuwa njia salama dhidi ya Juve leo ambao watahitaji kushambulia mda wote kutafuta matokeo ktk dimba la nyumbani.

For more/ Ushauri::
Choikangta.ckt@gmail.com

0 comments:

Post a Comment