Facebook

Friday 10 April 2015

Wanamitindo wembamba wapigwa marufuku.

Bunge la Ufaransa limeidhinisha sheria inayopiga marufuku tabia ya
makampuni ya wanamitindo nchini humo kutumia wasichana waonesha
mitindo walio wembamba kupita kiasi.
Sasa itabidi wanamitindo wembamba kuonyesha kuwa wanauzito wa
viwango vinavyokubaliwa kiafya.

Mawakala wa wanamitindo watakaokiuka viwango vilivyowekwa
watapigwa faini huku wakuu wa makampuni husika nao huenda
wakakabiliwa na vifungo vya hadi miezi 6.
Pia sheria imepitishwa inayopendekeza hatua kuchukuliwa dhidi ya
mitandao inayopendelea kuonyesha picha za wasichana walio
wembamba kiasi cha kudhoofisha kiafya.

0 comments:

Post a Comment