Facebook

Friday 10 April 2015

Walcott,Sterling kubadilishana timu.

Jarida la Starsport limebainisha kuwa Liverpool na Arsenal zinapanga
makubaliano ambayo yatazifanya timu hizo mbili kubadilishana
wachezaji wawili wa taifa la Uingereza.
Liverpool inahitaji pauni millioni 20 kwa nyota wake Sterling pamoja
na mchezaji wa Arsenal Theo Walcot kwa mpango huo kukubalika.
Walcott angejiunga na Liverpool msimu uliopita iwapo Luis Suarez
angejiunga na Arsenal.

Mkufunzi wa Arsenal Arsene Wenger alikuwa tayari kumuachilia
Walcott kujiunga na Liverpool lakini Suarez akabadili nia na kujiunga
na Barcelona.

Sasa mpango kama huo umeanza kuandaliwa huku Sterling mwenye
umri wa miaka 20 akipendelea kujiunga na Arsenal naye Walcott
akikosa fursa ya kuanzishwa katika kilabu ya Arsenal.

0 comments:

Post a Comment