Facebook

Sunday 12 April 2015

UCHAMBUZI WA MECHI ZOTE KALI ZA LEO J'PILI LIGI KUU UINGEREZA NA Mr CHOI (KWA TAARIFA YAKO)

QPR vs CHELSEA 15:30
        Tukianzia pale Loftus road ktk debi ya magharibi mwa jiji la London Qpr iliyo chini ya Ramsey ikiwa na point 26 nafasi ya 18 wata wakabili vinara Chelsea walio na point 70 .
     Kikubwa ni kuepuka kushuka daraja hali si shwari kwa upande wao licha ya kuwa na baadhi ya wachezaji wazuri wakiongozwa na mshambuliaji Austin mwenye magoli 17.
      Kwenye michezo 12 dhidi ya timu za London wamepata sare 3 tu na kufungwa michezo 9 na ushindi wao wa mwisho ilikuwa 2013 mwezi wa kwanza dhidi ya Chelsea kwa goli la Wright Philips.
    Qpr wamekuwa wazuri hasa ktk mipira ya juu na makosa mengi ya safu ya ulinzi ndiyo hupelekea matokeo mabovu, kiungo Philips ambae tangu mwaka huu uanze ndie bora ktk pasi za mwisho ndie mtu ambaye Chelsea watahitajika kumchunga sana.
       Mchezo wa 700 tangu Abramovich atue Chelsea 2003,pia utakuwa mchezo wa 100 kwa mchezaji bora mpaka sasa wa Chelsea Hazard huku safu yao ikitafuta goli la 100 ktk mashindano yote msimu huu.
    Costa hatocheza hivyo tutaraji kumuona Remmy na kikubwa hasa Chelsea wanatakiwa kuwa makini sana kwani uchezaji wa Qpr hauto kuwa tofauti na mchezo ule wa Hull city, bado kumekuwa na makosa madogomadogo ktk safu ya ulinzi ya Chelsea hasa kitu ambacho kilijitokeza ktk mchezo wa Hull na leo wasisahau kuna Austin mshambuliaji wa Qpr aliye bora ktk kila engo.

-----------
MAN UTD vs MAN CITY 18:00
        Pale machinjioni vijana wa Van Gaal walio ktk ubora mzuri huku wakishinda michezo 5 iliopita ambayo wengi hawakutaraji kama wata toka yote leo mbele ya City walio ktk kiwango kibovu kabisa.
     Ukiachilia mbali matokeo mazuri pia kuna wachezaji ambao wamekuwa ktk kiwango cha hatari ambao tutaraji wakiendeleza ubora huo mbele ya City leo nao ni Blind, Herrera, Mata kiukweli wamekuwa na mchango mkubwa ktk michezo ya hivi karibuni akiwemo mtu mzima Carrick.
    Ushindi ktk mchezo huu utaweka gepu la pointi 4 dhidi ya City kitu ambacho kitaongeza asilimia kwenye mbio zao za kucheza Uefa msimu ujao.
    Pellegrin siku zinavyo zidi kwenda ndivyo asilimia za kubaki Etihad zinazidi kupungua kutokana na matokeo mabovu aliyo yapata tangu January amekuwa hana mbinu mbadala ya kutafuta matokeo pindi timu ikizidiwa na kwa namna moja au nyingine uwepo wake na ukitizama uwepo wa Mancin kipindi kile akiwa kocha wa City bado hakujawa na utofauti mkubwa kati yao endapo atatimuliwa kuna haja ya kutafuta kocha alie na utofauti kulingana na hawa wawili.
      Watacheza mchezo huu wakiwa na presha kubwa walau kufufua matumaini ya ubingwa na presha walio nayo wasipo kuwa makini watajikuta wakipoteza mchezo huu.
        Watajaribu kuitafuta historia kuwa timu ya kwanza Epl kuifunga Man Utd mara 5 kwani mpaka sasa Utd kapoteza pointi 3 ktk michezo 4.
     Lazima mchezo utakuwa wa spidi kwa kila timu isipo kuwa umakini wa safu zote za ulinzi ndo zita amua matokeo.
    Aguero amekuwa mwiba kwa Utd kwani ktk michezo 3 ya timu hizi kafunga goli 4.
      
         3-Man Utd-62
         4-Man City-61

For more/ Ushauri::
Choikangta.ckt@gmail.com

0 comments:

Post a Comment