Facebook

Sunday 12 April 2015

UCHAMBUZI WA MECHI KALI YA LEO MANCHESTER DERBY.

Haukuwa mwanzo mzuri kwa Manchester united. Ndani ya dakika 10 za mwanzo Manchester City walionekana wazuri zaidi waliweza kupata goli la mapema na kukosa magoli mengine matatu ya wazi.

Kitu kikubwa ambacho naamini Manchester United ilikuwa silaha yao kubwa kwa leo ni hali ya hewa ya uwanja.Wakati timu uwanjani ikiwa na mwanzo mbaya lakini mchezaji wa kumi na mbili alikuwa kwenye ubora kabsaa.
Kuna wakati ulifika ukiangalia jukwaani na ukarudisha jicho lako uwanjani picha utakayoipata ni ile Manchester United ya mzee Sir Alex.Ilikuwa Manchester united yenye hasira, nguvu na ari kubwa ya ushindi.

Wakati unapoisifia Manchester United kwa kushambulia vizuri usisahau pia kuisifia jinsi ilivyokuwa inakaba vizuri.
Ilikuwa inakaba vizuri nafasi.Kuna wakati nilikuwa naiona Manchester City iliyokosa njia za kupitishia mipira. Na mipango yote hii iko chini ya Carrick.Yeye ndiye aliyekuwa anaamua timu ikabe vipi, timu ishambulie vipi. Mipango yote ya Carrick ilikuwa inasimamiwa vizuri na HERERRA.

Leo inaweza ikawa siku bora kwa Ashley YOUNG pamoja na kwamba alifunga goli moja pia amehusika kwenye upatikanaji wa magoli 3.

Upande wa kushoto wa Manchester united umeimarika zaidi baada ya Blind kuanza kuchezeshwa eneo la kushoto.

Inawezekana ilikuwa mechi nzuri kwa SERGIO AGUERO baada ya kuifungia timu yake goli la 100 la mashindano yote pia akifunga goli la 6 kwenye michezo 4 iliyopita iliyowakutanisha Manchester united na Manchester city.
Kitu kikubwa ambacho hakikuwa bora kwa Manchester City ni ile hali ya wachezaji wake kuchoka.

Kumbuka tangu msimu uliopita imetumia nguvu nyingi sana kupata ubingwa .Kikosi kile kile cha msimu uliopita ndicho hiki hiki kilichotumia nguvu nyingi mwanzoni mwa msimu kupata matokeo. Na mwisho wa siku wachezaji wanaonekana wamechoka na wengi wao umri umeenda na wamekutana na timu ambayo ndiyo iko kwenye ari ya ushindi ina uwiano mzuri wa umri wa wachezaji, timu ambayo haikuwa na michuano mingi msimu huu wachezaji wanaonekana miili yao ndiyo imefunguka inahitaji kucheza.Ndiyo maana baada ya kuwa wazuri dakika 18 za mwanzo , Manchester united ndio waliingia kwenye mchezo na city ndio walikuwa wanatoka kwenye mchezo.

Nahisi mabadiliko ya Kumtoa Vincent Kompany na Kumwingiza Mangala , kocha Manuel Pellegrini alifanya mabadiliko kwa kuogopa  Vincet kupata Kadi nyekundu. Ila kama angekuwepo mpaka mwisho angekuwa msaada mkubwa kuzidi Mangala.

Wakati city walipokuwa na Mangala hawakuwa na vitu viwili uwanjani.Cha kwanza kiongozi wa timu.Cha pili kiongozi wa safu ya ulinzi.Tumezoea Vincent kutumika zaidi kusahihisha makosa binafisi ya Martin.Unamwingiza Mangala mwenye makosa binafsi akiwa uwanjani, safu yako ya ulinzi wa kati inakuwa na mabeki wenye kufanya makosa binafsi, nani atakuwa anasahihisa makosa ya mwenzake?

MWISHO: Manchester united ya leo ilikuwa bora zaidi ya Manchester city ya leo.Unaweza ukawazungumzia utakavyo wakina Young, Blind, Herrera , Mata, Carrick, De gea, Valencia na wengine kwenye timu ya Manchester united ila kati ya mtu ambaye ana msaada mkubwa katika kuharibu mipango ya timu pinzani kuanzia kwenye nusu ya eneo la wapinzani mpaka kwenye nusu ya eneo la timu yake ya Manchester united basi ni FELLAINI..

Imeandaliwa na......
                             Martin Kiyumbi.

0 comments:

Post a Comment