Facebook

Friday 10 April 2015

Haya ni Matukio 10 makuu baada ya mauaji Garissa

Familia za wanafunzi 142 kati ya watu 148 waliouawa katika
shambulizi la kundi la wapiganaji wa Kiislamu Al Shabaab katika chuo
kikuu cha Garissa wameruhusiwa kuchukua miili ya wapendwa wao.

Familia zimeanza harakati za safari ya mwisho ya wapendwa wao
baada ya serikali ya Kenya kuwaruhusu kuzichukua miili kutoka
kwenye hifadhi ya maiti ya Chiromo jijini Nairobi.
Huu hapa mukhtasari wa matukio baada ya shambulizi hilo.

1.Shambulizi
Takriban wanamgambo 5 wa kundi la wapiganaji wa Kiislamu Al
Shabaab washambulia chuo kikuu cha Garissa alfajiri.
Waliwapata wanafunzi wakiwa wamelala.
Waliingia chuoni baada ya kuua walinzi wawili langoni.
Walionusurika wanasema kuwa wavamizi hao waliwabagua wanafunzi
waislamu na kuwaua wakristu.
Misa ya wafu huko Garissa

2.Uhuru ahakikisha taifa
Serikali ilitangaza kuwa watu 70 walikuwa wameripotiwa kuuawa na wengine 79 kuripotiwa kujeruhiwa.
Waziri wa usalama wa taifa generali mstaafu Joseph Nkaissery alitangaza idadi ya waliouawa kuwa ni 148 na kusema kuwa operesheni ilikuwa imekamilika

3.Idadi ya waliouawa yatangazwa
Wanafunzi 500 wameokolewa na maafisa wa usalama
Rais Uhuru Kenyatta ahutubia taifa na kutuma risala za rambirambi
kwa wale waliouawa.
Serikali ilionyesha hadharani miili ya wanamgambo waliouawa na
kuonyesha picha ya raia mmoja kutoka Tanzania aliyekamatwa.

Rais Uhuru Kenyatta atangaza kuwa Serikali yake itachukua hatua
kali dhidi ya wakenya wanaolisaidia Al Shabaab.
Serikali yakiri kuwa mmoja kati ya washambuliaji hao alikuwa ni
mwanawe Chifu wa kata ya Mandera.
Chifu huyo yamkini alikuwa ameripoti kwa polisi kuhusu kutoweka kwake mwaka uliopita.

4.Maswali yaibuka kuhusu Operesheni
Maswali yaibuka kuhusu hatua zilizochukuliwa na polisi baada ya
kuarifiwa kuhusu shambulizi hilo.
Wananchi waizomea serikali kwa kutumia ndege kuwasafirisha waziri
wa usalama wa taifa Joseph Nkaissery na Inspekta mkuu wa polisi
Joseph Boinett
huku kikosi maalum cha kupambana na magaidi al maarufu (RECCE)
kikilazimika kusafiri kwa gari kwa zaidi ya saa saba.
Wanafunzi walionusurika
Kikosi hicho kilitumia chini ya dakika 15 pekee kukamilisha operesheni
hiyo.

5.Makurutu 10,000
Rais Uhuru Kenyatta atangaza kuwa makurutu 10,000 wa polisi
waliokuwa wamepigwa marufuku na mahakama kufuatia madai
Waliotekeleza shambulizi la Garissa watajwa
ya rushwa sasa hawatakuwa na budi ila kuingia katika chuo cha
mafunzo ya Polisi ilikuimarisha idadi ya polisi na vilevile usalama wa
taifa.
Mahakama ilikuwa imeharamisha kusajiliwa kwao kufuatia madai ya
rushwa katika usajili.

6.Waliotekeleza Shambulizi watajwa
Raia wa Kenya Mohamed Kuno kwa jina jingine Mohamed
Dulyadin,atajwa kuwa ndiye mshukiwa mkuu.
Serikali ya Kenya imetoa ruzuku ya shilingi milioni 20 za Kenya yaani
dola $215,000 za kimarekani.
Taifa lahuzunika
Kuno aliwahi kuwa mwalimu katika eneo la Garissa kabla ya kustaafu
na kujiunga na kundi hilo.
Mwengine aliyetajwa ni wakili Abdirahim Abdullahi aliyeongoza
uvamizi huo.
Wanafunzi walionusurika Rais Uhuru Kenyatta aonya kuwa wale
wanaoendeleza sera za Al Shabaab wako miongoni mwa wakenya.

7.Maiti yaletwa Nairobi
Manusura waliopatikana wamelala
Maiti ya wahanga wa mauaji hayo yaletwa mjini Nairobi kwa ndege
za kijeshi.
Wale walionusurika pia wasafirishwa kwa msafara wa mabasi hadi
mjini Nairobi.
Kituo cha kuwapokea waathiriwa wa mauaji hayo na jamaa zao
kinaundwa katika uwanja wa michezo wa Nyayo mjini Nairobi.
Wale walionusurika pia wasafirishwa kwa msafara wa mabasi hadi
mjini Nairobi
Orodha ya wanafunzi waliouawa na wale waliojeruhiwa inapachikwa
katika lango la uwanja wa Nyayo.

8.Serikali yafunga miundo mbinu ya uchumi wa Al Shabaab
Serikali ya Kenya yatangaza orodha ya mashirika kumi na tatu na
akaunti za watu
binafsi wapatao 86 wanaoshukiwa kuhusika na ufadhili wa kundi la
kigaidi la Al Shabaab Garissa.
Akaunti za watu hao ambao zimesitishwa ni baadhi ya watu
waliokuwa katika orodha ya serikali ya Kenya ambao walikuwa
wakifuatiliwa mienendo yao.
kampuni 13 za ubadilishaji na usafirishaji wa fedha nazo zimefungwa.
Maafisa wa Polisi wakishika doria
Jamii ya wasomali yalalamikia hatua hiyo ikisema ni mtego ambao
umenasa waliokuwemo na wasiokuwemo.

9.Utambuaji wa maiti Chiromo
Shughuli ya utambuaji wa maiti yaanza huku familia nyingi
zikitatizika kutambua miili ya wapendwa wao kufuatia kuharibiwa
kabisa kwa miili.
Miili mingi ilikuwa na majeraha ya risasi kichwani.
Serikali ya Kenya yalazimika kutumia mashine maalum ya kutambua
chembechembe za damu za DNA ili kuharakisha utambuzi wa miili.
Dukuduku zaibuka kuhusiana na kuwepo kwa idadi kubwa ya wazazi
ambao wamekosa miili ya wapendwa wao.
Muungano wa walimu na wafanyikazi wa vyuo vikuu (UASU) yadai
kuwa takriban wanafunzi 166 hawajulikani waliko.

10.Uhuru aomboleza
Rais Uhuru Kenyatta aliwaandikia familia ya wahasirika wote
barua ya kuomboleza
Rais Uhuru Kenyatta jana aliwaandikia barua kila familia iliyopoteza
mpendwa wao.
Wote walioathirika walipewa shilingi laki moja za Kenya,Jeneza na gari
la kusafirishia maiti hadi makwao.
Makumi ya raia wa kigeni wakamatwa kote nchini kufuatia msako
mkali unaoendelea

0 comments:

Post a Comment