Facebook

Wednesday 29 April 2015

Jeshi la Nigeria lawaokoa watoto wa kike 293 kutoka katika kambi ya Boko Haram.

Jeshi la Nigeria limesema limewaokoa watoto wa kike mia mbili na
akina mama tisini na tatu kutoka katika kambi ya Boko Haram iliyoko
katika msitu wa Sambisa, kaskazini mashariki mwa nchi hiyo.

Jeshi hilo limesema watoto hao waliokolewa si kati ya wale waliotekwa
mwaka mmoja uliopita na kundi la kiislamu katika eneo la Chibok.
Jeshi limesema ya kwamba wanawake na watoto hao wa kike
walikutwa katika kambi nne tofauti ambapo silaha pia
zimekamatwa,Msemaji wa jeshi amesema waliwapata wasichana hao
baada ya kuziharibu kambi hizo.
"ni muda mfupi tu uliopita, wanajeshi wetu wameingia katika msitu
wa Sambisa, kutokea upande wa Alafa, ambapo walikuta kambi nne
zinazomilikiwa na wapiganaji na kuziharibu, hapo ndipo walipogundua
kuwa kuna wasichana wapatao mia mbili na wanawake tisini na tatu."
Jeshi la Nigeria
Kwa sasa jeshi limezuiwa kutoa utambulisho wa wasichana hao. Hata
hivyo, jeshi limethibitisha kwamba wasichana hao sio wale wanafunzi
waliotekwa katika mji wa Chibok.
"tuko katika mchakato wa kuwachunguza hawa wasichana ili tuweze
kubaini utambulisho wao, lakini kitu kimoja nataka nikiweke wazi kwa
umma, tunapotaja idadi ya wasichana mia mbili, tayari watu
wanaanza kufikiria wasichana mia mbili wa Chibok waliotekwa mwaka
jana, hawa sio wasichana wa Chibok, tutaendelea kuwajuza kadri
muda unavyokwenda iwapo kutakuwa na taarifa zozote. "

0 comments:

Post a Comment