Facebook

Friday 10 April 2015

Vatican wamkataa balozi kutoka Ufaransa kutokana na tuhuma za ushoga.

Mzozo wa kidiplomasia umezuka kati ya makao makuu ya papa
mtakatifu ya the Vatican na Ufaransa kuhusiana na uteuzi wa balozi
mpya wa Ufaransa, mjini Rome.
Rais wa Ufaransa Francois Holland, amempendekeza muumini mmoja
wa kanisa hilo ambaye ni mpenzi wa jinsia moja kuwa balozi wake
mjini Vatican.
Lakini utawala wa Vatican umesema uteuzi huo haukubaliki.

Makao makuu ya papa mjini The Vatican hayajasema lolote kuhusiana
na uteuzi huo ,lakini ni dhahiri kuwa baadhi ya maafisa wakuu katika
kanisa hilo hawajakubali msimamo wa papa kuhusiana na waumini wa
kanisa hilo ambao ni wapenzi wa jinsia moja.
Papa alinukuliwa akihoji kuwa yeye hawezi kumhukumu mtu yeyote
kwa misingi yoyote.

Makao makuu ya kanisa katoliki ,the Vatican
Serikali ya Ufaransa ilimteua laurent Stefanini kuwa balozi wake
mjini vatican mnamo mwezi Januari mwaka huu.

Balozi Stefanini mwenye umri wa miaka 55,amekiri hadharani kuwa
yeye anashabikia mapenzi ya jinsia moja na amewahi kufanya kazi
katika ubalozi huo mjini Roma na amekuwa mshauri wa masuala ya
kidini katika wizara ya mambo ya nje ya ufaransa.
Kwa sasa hakuna upande unaoonekana kuwa tayari kubadili msimamo
wake.

Ufaransa ilhalalisha ndoa za jinsia moja mwaka 2013 na uamuzi wa
The vatican wa kukataa kumkubali balozi Stefanini huenda ikawa ni
thibitisho la The vatican la kutoidhinisha msimamo huo wa Ufaransa.

0 comments:

Post a Comment