Facebook

Friday 10 April 2015

Somalia yatangaza majina 11 ya viongozi wa Al Shabab.

Serikali ya Somalia imetangaza ruzuku ya dola milioni moja kwa
yeyote atakayeisaidia kuwakamata viongozi 11 wa Al Shabaab.

Orodha hiyo ya watu 11 wanadaia kuwa viongozi wa ngazi ya juu ya
katika kundi hilo la wapiganaji wa wa kiislamu wa Al shabaab.

Kiongozi wa kundi hilo la wapiganaji Ahmed Diriye anaongoza katika
orodha hiyo huku Serikali ikitoa ruzuku ya dola laki mbili u nusu ($250,000) kwa yeyote atakayetoa habari zitakazofichua aliko.

Kitengo cha wanawake cha Al Shabaab
Jumla ya dola milioni moja zimetengwa katika hatua hii ambayo inalenga kuchochea umma kuisaidia serikali hiyo kuitokomeza
kundi hilo linalolaumiwa kwa mauaji ya zaidi ya wanafunzi 148 wa
chuo kikuu cha Garissa nchini kenya.
Orodha
Kundi hilo linalolaumiwa kwa mauaji ya zaidi ya wanafunzi 148 wa
chuo kikuu cha Garissa nchini kenya

Al Shabaab ambayo imetangaza wazi kushirikiana na wapiganaji wa kundi la Al-Qaeda wameahidi kuendelea kuishambulia Kenya hadi serikali hiyo itakapoondoa majeshi yake nchini Somalia.

Majeshi ya Kenya ni miongoni mwa wanajeshi wa muungano wa
Afrika .
Kundi hilo linataka Kenya iondoe majeshi yake nchini Somalia
Majeshi ya Muungano huo inashikilia maeneo mengi ya mijini kwa
ushirikiano na majeshi ya Serikali ya Somalia huku
kundi hilo la Al Shabaab ikitawala maeneo ya mashambani kusini mwa
taifa hilo ambalo limekuwa bila serikali kwa zaidi ya miongo miwli
sasa.

0 comments:

Post a Comment