Facebook

Tuesday 14 April 2015

Rais Kikwete:"Sijaletewa majina ya waliohukumiwa kunyongwa."

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Jakaya Mrisho Kikwete amesema kuwa hajaletewa majina ya watu 16 waliohukumiwa kifo kutokana na mauaji ya
maalbino nchini kwa sababu safari ya kisheria ya majina hayo kufikishwa kwake ni ndefu.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Jakaya Mrisho Kikwete amesema kuwa hajaletewa majina ya watu 16 waliohukumiwa kifo kutokana na mauaji ya
maalbino nchini kwa sababu safari ya kisheria ya majina hayo kufikishwa kwake ni ndefu.
Rais Kikwete aliyasema hayo jana, Jumapili, Aprili 12,2015 wakati alipozungumza katika ibada maalum ya kuwekwa wakfu na kusimikwa kwa Askofu Liberatus Sangu kuwa Mhashamu Baba Askofu wa Jimbo la Kanisa
Katoliki la Shinyanga.

Akizungumza katika ibada hiyo iliyofanyika kwenye
Kanisa Kuu la Mama Mwenye Huruma, Ngokolo, mjini
Shinyanga na mbele ya viongozi wengi wa Kanisa hilo
wakiwemo maaskofu wakuu, maaskofu na maaskofu
wasaidizi 38, Rais Kikwete alitumia nafasi hiyo kujibu
madai kuwa Serikali yake haichukui hatua za kutosha
kukabiliana na mauaji ya albino na pia kufafanua juu ya
shinikizo ambalo linatolewa na baadhi ya mashirika
yasiyokuwa ya serikali (ngo’s) yakimtaka Rais kutia saini
ya kuruhusu watu hao wanyongwe.
Rais Kikwete aliwaambia viongozi hao wa dini: “Ninayo
maombi maalum kwenu viongozi wa dini. Naomba
mtusaidie kuielimisha jamii ili iachane na imani za
kishirikina. Vikongwe wanauawa kwa sababu tu ya kuwa
na macho mekundu na ujinga uliokithiri unaosababisha
Watanzania wenzetu wenye ulemavu wa ngozi (albino)
kusakwa na kuuawa kikatili kabisa.”
“Nawaombeni sana viongozi wa dini tusaidiane katika
kukomesha ujinga huu mkubwa kwa kutoa elimu kwa
waumini wenu, ili wajue kuwa vikongwe wana macho
mekundu kwa sababu ya kutumia samadi ya ng’ombe
kupikia kwa muda mrefu na kuwa kiungo cha albino
hakiweza kuleta utajiri wowote,” Rais aliwaambia viongozi
hao wa dini.
Kuhusu madai kuwa Serikali yake haichukui hatua za
kutosha kukabiliana na mauaji ya albino, Rais Kikwete
aliwaambia viongozi hao: “Tumewatia mbaroni watuhumiwa
wengi wa mauaji ya albino. Watu 16 tayari
wamehukumiwa kifo na wengine wanasubiri…kesi zao
zinaendelea kusikilizwa. Yapo maneno maneno, lakini
binafsi kama Rais sijaletewa majina ya watu hao.”
Aliongeza: “Ni lazima tuelewe jinsi mfumo wetu wa kutoa
haki unavyofanya kazi hasa katika eneo hilo la kunyonga
ama kutokunyonga. Ni mlolongo mrefu. Katika kesi za
watu kuhukumiwa kifo, kwanza kukata rufani ni lazima na
wala siyo jambo la hiari ama matakwa ya aliyehukumiwa.
Pili, tukimalizana na rufani ni lazima Kamati ya Msamaha
(Committee on Prerogative of Mercy) nayo ifanye kazi.
Kwa hiyo ni utaratibu mrefu kidogo.”
Mhashamu Baba Askofu Sangu ambaye aliteuliwa na
Baba Mtakatifu Francesco kuwa Askofu Februari 2,
mwaka huu, 2015, amechukua nafasi ya hayati Baba
Askofu Aloysius Balina ambaye alifariki dunia Novemba 6,
2012.
Wakati wa uteuzi wake, Mosinyori Sangu alikuwa
anafanya kazi kwenye Idara ya Uenezaji Injili
Ulimwenguni katika makao makuu ya Kanisa Katoliki,
Vatican ambako alifanya kazi kwa miaka minane.

0 comments:

Post a Comment