Facebook

Sunday 19 April 2015

"DERBY DELLA MADONNINA" INTER MILAN vs AC MILAN

       Kila kitu huwa kina mwanzo na mwisho wake lakini upande wa soka hasa kwa vilabu mwisho wake unakuja pindi timu inapo shindwa kujenga misingi imara yenye muendelezo wa kubaki ktk kiwango cha juu.
    Ukizungumzia Real Madrid ni miongoni mwa vilabu vikongwe Duniani vilivyo fanikiwa kujenga misingi bora endelevu ndo mana imekuwa ngumu kwa wao kushuka kirahisi.
    Kikubwa hasa naangazia mchezo wa siku ya leo ktk ligi kuu Nchini Italy ambapo tutashuhudia Nerazzurri wakichuana na Rossonery kwenye dimba la Giussepe d Meaza ( Sansiro ).
    Miaka kadhaa iliopita mchezo huu uliteka hisia kubwa za mashabiki wa soka Duniani kote kulingana na ubora wa vikosi vyao ulivyo kuwa ukichagizwa na mvuto wa Serie A.
    Lakini kutokana na kutokuwa na misingi imara  endelevu kwa timu hizi kukichagizwa na sekeseke la uchumi bila kusahau kashfa za upangaji matokeo ktk ligi yao mchezo huu umebaki kutizamwa na wanahistoria ama wadau halisia wa timu hizi wengine wanaona hakuna jipya zaidi ya kukumbushiwa machungu ya utamu halisia wa timu hizi enzi zileee.
      Timu zote zimekuwa zinawachezaji wa kawaida, ushindani wa kawaida na ukijaribu tizama nafasi waliopo kwenye msimamo utaelewa viwango vyao ni sawa hivyo kuwafanya Juventus kuwa taswira ya Italy kwa mbali Lazio,Roma na Napoli wakifuatia.
     Mpaka hivi sasa wenyeji wa mchezo wa leo Inter wapo nafasi ya 10 kwa pointi zao 41 kwenye ligi huku ndugu zao wakiwa nafasi ya 9 kwa pointi 42 ni tofauti ya pointi moja tu kati yao kitu ambacho kitapelekea ugumu wa mchezo huu.
   Wamesha cheza michezo 162 ya ligi Nerazzurri wakishinda michezo 60 dhidi ya 50 kwa wapinzani wao na kumekuwa na sare nyingi kwa kipindi cha hivi karibuni pindi wakikutana mara ya mwisho ilikuwa 1-1 na kufungana kwao ni Inter kuibuka na ushindi wa goli 1-0 2013 kwa goli la Palaçio.
    Mara ya mwisho timu hizi zilipokutana ushindi wa idadi kubwa ya magori ulikuwa msimu wa 2012 kwa Inter kuwachabanga Ac 4-2 zaidi ya hapo kumekuwa na ufinyu wa wingi wa magoli.
     Pengine hawa ndio watakao anza kwenye mchezo huu kwa pande zote.
      Inter Milan:Handanovic, Santon, Ranocchia, Vidic, Juan Jesus, Hernanes, Medel, Kovacic, Shaqiri, Icardi,Palacio.
     AC Milan possible starting lineup:Lopez, Abate, Mexes, Paletta, Antonelli, Poli, De Jong, Van Ginkel, Cerci, Bonaventura, Menez

     Mechi saba za hivi karibuni Ac milan imefungwa mara 4 huku wakitoa sare 2 na kushinda mchezo 1 kumekuwa na takwimu za kulingana ndani ya dimba zikutanapo kwa upande wa umiliki
      Umakini kwa Giacomo Bonaventura utahitajika ktk safu ya ulinzi ya Inter pia Palaçio kwa upande wa Ac milan.
     Nadhani na wewe utizame mchezo huu ambao kwa kuangalia historia zao kuna haja ya kuutizama tuone ni Mancin au Inzagh.

For more/ Ushauri::
Choikangta.ckt@gmail.com

0 comments:

Post a Comment