Facebook

Monday 23 March 2015

NICASIUS COUTINHO SUSO:- MAMBO KUMI NILIYOJIFUNZA BAADA YA EL CLASSICO.

1. Kama kuna mtu mshale wake wa saa unaenda mbio kuliko wote duniani basi kabla ya Falcao ni Gareth Bale. Huyu kasharudisha chenji ya Perez katika misimu miwili hii,  usitegemee kafara itamhusu mtu tofauti na yeye. Hata mimi binafsi sijaridhishwa na kiwango chake siku za karibuni achilia mbali ujinga wa Ronaldo dhidi yake. Hata yeye atakuwa anaitizama miwani ya Perez kwa umakini kuliko anavyomtizama mpenzi wake Emma Rhys Jones kwa husuda.

2. Ukishakuwa na Messi ndani unakuwa na wachezaji watatu kwa Sasa wa ziada ndani yake na yeye wa nne,  unakuwa na winga, Kiungo mshambuliaji, Striker na jina lake mwenyewe ambalo ni hatari kuliko hivi vitatu vingine. Kumkaba huyu yataka moyo, vinginevyo ucheze mchezo mchafu tu wa madhambi. Madrid walivyofanya hivi kiasi walifanikiwa, Mancity hawakuwaza Hilo.

3. Luka Modric. Kipaji asilia. Huyu anakutana na tatizo kama la yule Bastian Schweinstiger. Dunia haina usawa kabisa, sio ajabu ukasikia Aaron Ramsey, Herrera, Henderson, Rakitic, na yule Oscar wanatajwa juu ya hawa. Acha Diamond aimbe Tatizo nyota wakati mwingine.

4. Huwezi kuwa/hapatokuwepo refa sahihi kuchezesha huu mchezo,  presha haianzii uwanjani kwa mashabiki zaidi ya 80 elfu katika viwanja vyao wote,  presha inakuja mpaka huku kwa mashabiki zaidi ya million tano wanaoutizama mchezo huu duniani, bahati mbaya hata wachezaji wanne ghali zaidi wapo huku. Napata shaka hata Perluig Collina kama angeweza kisawasawa.

5. Felipe Luis mbele ya Marcelo?  Uongo anaoutumia Dunga ni kama ule wa Loew kumuaminisha Poldoski ni mchezaji anayetakiwa timu ya taifa Ujerumani kwa Sasa. Tatizo kubwa la Marcelo lilikuwa ukabaji lakini kwa Sasa amekuwa moja ya mabeki bora wa ulinzi Pembeni, achilia mbali kuwa ndo beki bora zaidi linapokuja suala la ushambuliaji. Hata hivyo Ile staili yake ya siku ulinifurahisha zaidi, ilikuwa tamu kuliko goli la Suarez.

6. Kuna Neymar wawili duniani. Mmoja yupo timu ya taifa, mwingine Barcelona. Siku huyu wa Barcelona akimuiga tule wa timu ya taifa Brazil, basi Ana miaka miwili kuchukua Ballon D Or, akiwaacha Hawa wamalizie muda wao. Wakati huo namba tatu itakuwa yake.

7. Ningekuwa na mawasiliano na Anceloti ningemwambia tu, ni bora Israel wawaamini wapalestina kuliko yeye kumuamini Perez. Aachane na Mourinho akamuulize Capello baada ya kuchukua ubingwa nini kilifuata. Ni rahisi kufanya majadiliano na Abramovich kuliko huyu.

8. Isco...  Del Bosque Kuna kichwa tu. Kuna watoto wanakera sana,  wakati unamuwaza Silva,    Navas, Mata yeye anakupa sababu ya ulimwengu kukunyooshea kidole, kumuacha huyu kikosi cha kwanza achilia mbali timu ya taifa unatakiwa uwe na roho ya Hitler. Hata Anceloti najua anaumwa kichwa akirudi James itakuwaje.

9. Kareem Benzema, umefika muda sasa, umeshinda kila kitu katika klabu, waachie ufalme wao. Pishana na yule Falcao uende ukajichukulie ufalme pale Manchester au sogea pale Liverpool, si unamuona Sanchez. Hata akiwa katika kiwango kibovu mashabiki wanainama na kumsujudia. Alichokifuata Suarez Barcelona ndicho ulichonazo, na akichokipata Anfield ndicho unachokikosa. Kuitwa mfalme katika nchi inayokuhusudu.

10. De Gea endelea kugomea mkataba mpya United. Sio muda utatakiwa ukachukue Ile nafasi madrid, haina maana kuwa Casillas alicheza vibaya Ila unaona hata uhamasishaji wake golini umeshuka sana.

NB:
Usiniulize kwanini hayapo ya Manchester United vs Liverpool. Yule Mata kajibu makala yangu ya wiki iliyopita, Fellaini kajibu uchambuzi wangu wa sports bar na sports xtra. Hata hivyo yule Blind Hana adabu achilia mbali ubora wake ambao wengi hawausemi, Ile chenga alompiga Emre Can inahitaji uwe umesoma vizuri hesabu kuifanya na kuizuia. Wanaweza wanaotumia mikono tu (basketball).  Huu sio wakati mzuri kukutana na Man United, wanakaba vizuri kuanzia kwenye nusu yao, na wanatengeneza mgawanyo mzuri wa mashambulizi. Sema kinachokera Mata anaweza kurudi benchi au Herrera. Hapo tu.

Yule Gerrard napata shaka hata mechi ya kumuaga atakuwa na tukio yule.  

Siku Raheem akitaka tena 140 mwambieni haipatikani vile. Yule Coutinho mkataba waliompa unamlinda kuja kuondoka kwa kitita kikubwa.

Ahsanteni. By Nicasius Coutinho Suso

0 comments:

Post a Comment