Facebook

Saturday 19 April 2014

Soma hapa barua ya Jeshi la Polisi inayowazuia Upinzani (Ukawa) kutokufanya maandamano.........fuatilia hapa...........

. baruaaa 


Baada ya kugoma kuendelea kuhudhuria vikao vya bunge la katiba Dodoma, Umoja wa katiba ya Wananchi (UKAWA) unaoongozwa na Profesa Ibrahim Lipumba na Freeman Mbowe ulitangaza kufanya mkutano Zanzibar Jumamosi ya leo kuwaeleza wananchi kilichotokea ambapo baadae wangetembea nchi nzima.
Mkutano huo ilikua waufanye leo April 19 2014 ambapo kutokana na sababu za kiusalama zilizotolewa na Jeshi la Polisi Tanzania mkutani huo haukufanyika
     

                                                                       
                                          RAMADHANI S. NGAMIA – SS
                                          MKUU WA POLISI,
                                          WILAYA YA MAGHARIBI
 UNGUJA.

YAH: TAARIFA YA KUSITISHWA MKUTANO WA HADHARA


          Naomba urejee barua yangu Kumbu. Nam. W/MGH/SO/7/2/A/4 ya tarehe 17 Aprili, 2014 inahusika.
Ninakujulisha rasmi kuwa mkutano huo uliokuwa ufanyika  tarehe 19 Aprili, 2014 hapo Viwanja ya Demokrasia Kibanda Maiti umesitishwa kwa sababu za KIUSALAMA WA NCHI.

Kwa barua hii unatakiwa kuwajulisha Wanachama na wapenzi wote wa Chama kuwa watulivu kwa muda huu hadi hapo hali itakapo ruhusu kufanyika tena kwa mkutano huo.
Tafadhali nawasilisha.


Katika Taarifa ya habari iliyosomwa kupitia TBC1 imeeleza kuwa Jeshi la Polisi Zanzibar limesitisha mikutano yote ya hadhara ya vyama vya siasa visiwani humo ambapo hiyo imesemwa na kamishna wa Polisi Zanzibar Hamdan Omar Makame wakati alipokutana na viongozi waandamizi wa vyama vya CCM na CUF katika makao makuu ya Jeshi la Polisi Ziwani Zanzibar.
Kabla ya kutolewa tamko hilo UKAWA walipanga kufanya mkutano kama ilivyoelezwa hapo juu wakati UVCCM walipanga kufanya mkutano wa hadhara kesho April 20 Jumapili katika eneo la Mabata

Endelea kutembelea katemimethsela.blogspot.com kujua kila kinachojiri katika mchakato wa katiba mpya

0 comments:

Post a Comment