Facebook

  • Tutorial 1

    This is Trial

  • Tutorial 2

    This is slide 2 description. Go to Edit HTML and replace these sentences with your own words. This is a Blogger template by Lasantha - PremiumBloggerTemplates.com...

  • Tutorial 3

    This is slide 3 description. Go to Edit HTML and replace these sentences with your own words. This is a Blogger template by Lasantha - PremiumBloggerTemplates.com...

Wednesday, 30 April 2014

Adam Nditi:Niko tayari kuichezea Taifa Stars kama mtakubali uraia wa Nchi mbili...

051c57b47232e95173755dcfe596c530 copy
MCHEZAJI kinda wa klabu ya Chelsea na raia wa Tanzania, Adam Nditi ameilaumu serikali ya Tanzania kuwanyima haki watanzania wengi walio nje ya nchi kuja kuitumikia nchi katika fani mbalimbali kutokana na kushindwa kuruhusu uraia wa nchi mbili.
Katika mahojiano maalum, Nditi amesikitishwa na serikali kushindwa kutoa uraia wa nchi mbili kwasababu wanaona uchungu kuona nchi yao inafanya vibaya wakati wanao uwezo wa kutoa mchango wao.

“Binafsi kama serikali ya nchi yetu itaruhusu uraia wa nchini mbili, niko tayari kuja kuichezea taifa stars hata kesho”. Amesema Nditi.

Nditi ameendelea kufafanua kuwa wapo watanzania wengi wenye fani mbalimbali kama vile wanasoka, madakatari na nyinginezo, lakini wanashindwa kuja kuitumikia nchi kwasababu taifa halijakubali uraia wa nchi mbili.

“kinachowasumbua watu wengi ni maslahi wanayoyapa huku Ulaya”.

“Inakuwa ngumu kwa watanzania waliopo huku kuacha kazi zinazowalipa vizuri na kuja nchini”.

“Lakini kama suala la uraia wa nchi mbili litaruhusiwa, wengi watakuja”. Ameongeza Nditi.

Aidha, kinda huyo mwenye kipaji cha juu katika klabu ya Chelsea amesisitiza kuwa ifike wakati serikali iwafirie na kuukubali mfumo wa uraia wa nchi mbili kwani ni wajibu wa msingi kulisaidia taifa katika fani tofauti.

“Nchi yetu ina upungufu wa madaktari na wanamichezo bora, lakini wanashindwa kuja kusaidia Taifa”.

“Nasisitiza serikali ituruhusu na sisi tuje kuiokoa nchi yetu”. Amesema Nditi.

Nditi alizaliwa Zanzibar mwaka 1994 kabla ya kujiunga na timu ya Chelsea ya chini ya miaka 13 miaka kadhaa iliyopita baada ya kuhamia England na familia yake

Uchambuzi: Bayern Munich 0-4 Real Madrid


 
Ushindi wa Madrid wa bao 4-0 magoli mawili kila mmoja kwa Sergio Ramos na Cristiano Ronaldo yameivusha Madrid kwenda katika fainali ya Ligi ya Mabingwa Ulaya Mei 24 pale Lisbon Ureno kwa ushindi wa Jumla wa magoli 5-0.
KWA MATOKEO HAYO:-
> Real Madrid imefika fainali yake ya 13 tangu ianze kushiriki michuano hiyo huku ikiwa imeshachukua kombe hilo mara 9.
> Real Madrid licha ya kuwa timu yenye mafanikio na historia kubwa katika michuano hiyo wamesota miaka 12 mpaka kupata nafasi ya kucheza fainali mwaka huu mara ya mwisho ilikua mwaka 2002.
> Real Madrid ndo timu ya kwanza kuifunga Bayern 4-0 nyumbani kwao Alianz Arena katika mashindano yote mara ya mwisho kufungwa 4-0 nyumbani ilikua mwaka 1979
> Ronaldo amefunga goli lake la 16 msimu huu na kuvunja kabisa rekodi zote zilizowekwa awali na  Jose "Mazzola" Altafini wa AC Milan mwaka 1962/1963 na Lionel Messi mwaka 2011/2012.
>  kutolewa kwa Bayern Munich ambao wengi tuliamini angetetea taji hilo imepelekea Historia kuzidi kuendelezwa kwa bingwa mtetezi kushindwa kutetea taji lake katika michuano hiyo.
MIWANI PANA YA KATEMI:-
Mimi Katemi naamini Anachokifanya Pep Guadiola (Kocha wa Bayern) kuibadilisha Timu hiyo kiuchezaji imefanikiwa mno na bado kitambo kidogo Bayern itakua moto wa kuotea mbali ila atafanikiwa kama atapata mabeki wenye kasi na wanaoweza kupanda na kurudi kulinda lango hapa nawaona Laurent Koscienly wa Arsenal, Vicent Kompany wa Man City au David Luiz wa Chelsea kama wachezaji sahihi wa kuchukua nafasi ya Dante na Boateng katika safu ya ulinzi.
Real Madrid ina kila sababu ya kubeba ubingwa mwaka huu kwani ndo timu iliyokamilika kila idara kwa  miwani yangu paaaaaaana na kwahilo mpira tutakua tumeutendea haki.

Roy Hodson tayari anakikosi chake cha England cha Brazil............

ROY_HODGSON-29APR









MENEJA wa England, Roy Hodgson, tayari anajua ni Wachezaji gani 23 atakuwa nao huko Brazil kwenye Fainali za Kombe la Dunia zinazoanza Juni 12 na hatarubuniwa na fomu ya Mchezaji yeyote kwenye Mechi hizi za mwisho za Ligi Kuu England.
Akihojiwa na Wanahabari, Hodgson amesema tayari ana mipango thabiti kabla hajatangaza Kikosi chake cha Wachezaji 23 hapo Mei 13 na uchaguzi wake huo wa Wachezaji unazingatia fomu ya Mchezaji ya Miezi kadhaa na hata Miaka.
Amesema: “Hakuna kitu kitakachotokea Gemu hizi 4 za mwisho na Mchezaji kung’ara na kunibadilisha mimi. Siwapimi Wachezaji kwa hali zao za Dakika za mwisho kwenye Mechi 2 au 3! Napima Wachezaji kwa zaidi ya Miaka miwili. Na kama yuko mpya kaibuka basi nampima kwa Miezi kadhaa. Siwezi kufanya uamuzi kwa kutazama Wiki iliyopita tu na hii ni mbaya sana kupima vipaji!”
Aliongeza: “Nilishakuwa na fikra za wazi nini nataka kufanya na Kikosi hiki kwa muda mrefu sana. Hivi sasa najua wazi nini nataka kufanya na hii Timu.”
Hodgson ndie Meneja wa kwanza wa Kiingereza kuiongoza England kwenye Fainali ya Kombe la Dunia kwa Miaka 16 baada kuongozwa na Wageni kina Sven-Göran Eriksson, kutoka Sweden, kwenye Fainali za Kombe la Dunia Mwaka 2006 na kutolewa Robo Fainali, na kisha Fabio Capello wa Italy kwenye Fainali za Mwaka 2010 na kubwagwa nje Raundi ya Pili.
England, ambao wako Kundi D huko Brazil, wataanza Kampeni yao dhidi ya Italy hapo Juni 14 Mjini Manaus na kufuatia Mechi dhidi ya Uruguay na Costa Rica.

Je!! Unamjua Mbwa Mkubwa Zaidi Duniani........muangalie hapa...

dd dd 1

Anaaminika kuwa kwenye wanyama wa kubwa aina ya Mbwa basi huyu anawezekana kuwa mbwa mkubwa zaidi. Jina alilopewa na mmiliki wake ni Freddy na anaurefu wa futi 7 na nchi 4.
Mlo wake kwa siku una Kilo 6 anaishi Uingereza. 

Ronaldo azidi avunja rekodi Ulaya............

UCL-REKODI_YA_MAGOLI 
Cristian Ronaldo avunja rekodi na kuwa mchezaji aliyefunga magoli mengi kwenye michuano ya UCL ndani ya msimu mmoja..

Je unamjua msanii wa kwanza wa Bongo Fleva kupata Vevo Account....fuatilia hapa.....

downloadfile-1 

Gosberth Kibanza aka Gosby Mwanamuziki wa kizazi kipya mwenye hit mbalimbali kama Monifere na Video yake ya BMS ambayo ilivuka mipaka mpaka kituo cha chanel O ya Afrika Kusini amekuwa mwanamuziki wa kwanza wa kizazi kipya kuwa accepted na VEVO na kumpa account ya kuweka kazi zake za kimuziki.
vevo_logo_detailVEVO ni mtandao wa internet unaoshughulika na video za music na wanamuziki unaomilikiwa na kampuni kubwa za muziki duniani SONY Music Group, Universal Music Group, Warner Music Group na Google ,VEVO ni mtandao number moja duniani unahusika na kuhifadhi na kurusha kazi za muziki za wanamuziki maarafu duniani, kama Jay Z, D’banji, Nick Minaji, Mafikizolo na wengine wengi
Gosby 

Baada ya kupata Account hiyo ya VEVO Gosby amesema ’Nina furaha kubwa sana kwa kuwa mara nyingi nimekuwa natamani kuwa na account ya VEVO, VEVO ni platform kubwa ya wasanii na wadau wa muziki duniani’

‘Nafurahi kuwa miongoni mwao sina shaka kazi zangu zitatazamwa na wadau wakubwa wa soko la muziki afrika na dunia,yah unaweza kuwa na video zako youtube kama wanamuziki wengine au hata wasio wanamuziki lakini VEVO ni maalum kwa Established Musicians Only’
‘Hata mtu akitazama Music Video zako VEVO anakuwa na uhakiwa kuwa hii ni video ya Established artist, nadhani ni njia iliyosahihi kwa wanamuziki wa kizazi kipya hapa nyumbani kujaribu kupata VEVO accounts’
‘Wenzetu wa Afrika Magharibi na Afrika Kusini wanamuziki wao wote wakubwa wana VEVO accounts, mapinduzi yetu ya muziki yasiishiekwenye platform za hapa nyumbani tu, ila tutumie fursa zaidi za masoko na kujitangaza kwenye mitandao mikubwa duniani ili kuwa na wigo mpana zaidi wa kutangaza kazi zetu na nchi yetu’.

‘Imeichukua management yangu takribani mwezi mmoja na zaidi kufuatilia, kujaza ma form na finally kuwa accepted na VEVO inayopatikana kwenye Youtube.com na VEVO.COM, nichukue fursa hii kuipongeza management yangu kwa kazi nyingine bora na yakujivunia na vile vile nitumie fursa hii kuwapongeza mashabiki wangu kwa uvumilivu waliokuwa nao katika kipindi hiki cha ku-migrate kazi zangu kutoka youtube na kwenda VEVO ‘

‘video yangu ya BMS ilikuwa na Views 45,000 kipindi tunaishusha ili kuweza kuhamia VEVO ikiwa ni moja ya masharti ya VEVO ili kuzuia duplication”
 
Gosby pia ameongelea wimbo wake mpya anaotarajia kuutoa hivi karibuni aliomshirikisha Ommy Dimpoz 
"Yeah ninakazi nyingi ambazo ziko kwenye studio tofauti tofauti na ambazo nimefanya na producers tofauti tofauti kama 10 hivi na zimefanywa na producers tofauti kama 7 wa hapa nchini na nje ya nchi"

Davido naye apost picha akila ndizi...........



Amazing: Davido, Samuel Eto’o, Adebayor, Balotelli Post Banana Photos In Support


This awesome, this is amazing and breathtaking…. When I personally watched that video I was really touched…

Dani Alves ate the banana that was thrown at him, he started a revolution. Right now, it’s taken over the


social media.


The racist incident happened during Barcelona’s match against Villarreal on Sunday, when a banana was thrown onto the pitch towards Dani Alves as he went to take a corner. Everyone was amazed as Dani picked it up, peeled it back and ate it. And since then, he has been receiving massive support against racism.


Speaking after the match Alves said:


“We have suffered this in Spain for some time, you have to take it with a dose of humour. We aren’t going to change things easily. If you don’t give it importance, they don’t achieve their objective. I don’t know who it was, but thanks to whoever threw the banana, the potassium gave me the energy for the two crosses which led to a goal.”


The banana thrower has been identified and banned for life from games at the El Madrigal Stadium. The banana campaign for Alves has also gone viral. With even Davido sharing his own photo.. This is a nice move from Spanish F.A.. You wouldn’t want to try it in Nigeria, you will be beaten to stupor before banning of life.

Samuel Etoo naye ampa support Dani Alves........

Unaambiwa club ya Villareal imemfungia maisha yule shabiki ambae alionyesha kitendo cha kibaguzi kwa kumrushia ndizi Dani Alves, kitendo ambacho kilitafsiriwa kwa Alves kufananishwa na nyani.
Wachezaji kadhaa wamemsupport kwa ujasiri wake wa haraka na kula ndizi hiyo aliyotupiwa uwanjani alafu akaendelea na game kama kawaida ambapo miongoni mwa waliomsupport ni Neymar.

Mwingine alieonyesha support ni Samuel Eto’o ambae baada ya kuweka picha zake mbili akiwa kwenye magari yake ya kifahari na kuandika ‘samahani nilisahau kuuliza, kuna yeyote anataka kuwa nyani kama mimi?’


Costa:Najua Chelsea hawatapaki basi,watakuwa wanashambulia,lakini tutawafunga.....


397162_heroa MSHAMBULIAJI hatari wa Atletico Madrid, Diego Costa anaamini kuwa Chelsea hawatatumia mbinu yao ya kujilinda katika mchezo wa nusu fainali ya pili ya UEFA leo katika  uwanja wa Stamford Bridge.
Jose Mourinho alitumia mbinu ya `Kupaki basi` katika mechi ya kwanza uwanja wa Vicente Calderon na kulazimisha suluhu ya bila kufungana na alitumia mbinu kama hiyo kuwafunga Liverpool mabao 2-0 jumapili iliyopita katika mchezo wa ligi.

Hata hivyo, Costa mwenye uraia wa Hispania anatarajia kuona Chelsea ikishambulia zaidi katika mechi ya kesho jumatano kwa malengo ya kufika fainali.

“Sina shaka, ni mchezo mkubwa, acha tufurahi na kuucheza”. Costa amewaambia waandishi wa habari.

“Itakuwa mechi tofauti kwa wenyeji, watajitahidi kucheza kwa kushambulia zaidi”.

Atletico msimu huu wana uchu wa kutwaa ubingwa wa La Liga tangu walipofanya hivyo kwa mara ya mwisho mwaka 1996 na Costa ana ndoto ya kubeba kombe Calderon.

“Ninataka kushinda kombe la ligi na itakuwa furaha kubwa kufanya hivyo mbele ya mashabiki wetu tutakapokutana na Malaga”. Aliongeza.

Atletico Madrid katika mechi bili za mwisho watasafiri kuwafuata Levante na mchezo wa kufungia msimu watakutana na Malaga nyumbani

Mr.Blue awataja waliomfilisi........





NYOTA wa Bongo Fleva, Herry Samir maarufu kama Mr. Blue amesema wasichana warembo, Wema Sepetu na Najma ambao aliwahi kutoka nao kimapenzi kwa nyakati tofauti miaka ya nyuma, walimfilisi kutokana na matumizi makubwa ya fedha alipotoka nao viwanja.


Akizungumza na paparazi wetu hivi karibuni, Mr. Blue, msanii aliyeanza kupata umaarufu akiwa bado kijana mdogo, alisema alilazimika kutumia fedha nyingi akiwa nao, kwani vinginevyo wangemuona hana pesa, kitu ambacho hakuwa tayari kuona kinatokea.


“Mademu wengi walikuwa wanapenda sana starehe, kila day (siku) wanataka twende kiwanja, ndiyo maana kama unakumbuka niliyumba kimuziki.


“Wanawake wengi niliotoka nao hawajulikani, ila kuna Wema na Najma, ilikuwa ukizama nao dukani lazima ufanye shopping (manunuzi) ya nguvu, kuanzia laki saba, nane na kuendelea ili wakuone unazo na mademu wengi wakisikia tu umepiga shoo, sms hazikauki kuomba uwatumie mawe (pesa),” alisema.


Kuhusu maisha yake ya sasa, Mr. Blue alisema yamebadilika sana, kwani hivi sasa ameoa mwanamke mwenye asili ya Kiarabu na amejaliwa kupata mtoto mmoja, hivyo ni baba wa familia ambaye pia anakaribia kumaliza mjengo wake siku si nyingi.


Hata hivyo alisema mkewe siyo maarufu, ana malengo na upendo kwani amekuwa akimuaga kila safari anayofanya na kwamba hata yeye anaporejea nyumbani, hupokelewa vizuri.


Mr. Blue ni mmoja kati ya wasanii wa muda mrefu ambao bado wanafanya muziki na wenye mashabiki wengi ndani na nje ya Bongo.

UKAWA waruhusiwa kufanya mkutane Zanzibar leo hii...................



 







Hatimaye mkutano wa Umoja wa Katiba ya Wananchi (Ukawa), uliokuwa umezuiwa kupisha sherehe za Muungano utafanyika leo katika Viwanja vya Kibandamaiti, Unguja baada ya kupata baraka za polisi.

Mkutano huo awali ulikuwa ufanyike Aprili 19, mwaka huu lakini ukazuiwa na polisi kwa maelezo kuwa intelijensia yao ilionyesha kuwa kungekuwa na tishio la maisha ya watu. Hivyo walishauriwa wapange tarehe nyingine baada ya Sikukuu ya Pasaka.


Hata Aprili 23 ambayo ilikuwa imepangwa kufanyika kwa mkutano huo, ilikataliwa na polisi kwa madai kwamba askari na maofisa wa jeshi hilo walikuwa Dar es Salaam katika maadhimisho ya miaka 50 ya Muungano yaliyofanyika Aprili 26, mwaka huu.


Msemaji wa Polisi Zanzibar, Mohamed Mhina amethibitisha kuruhusiwa kwa mkutano huo na kuwataka wananchi watakaohudhuria kuwa watulivu kabla na baada ya mkutano.


“Tumewaruhusu kufanya mkutano huo lakini maandamano hayataruhusiwa kufanyika,” alisema Mhina.


Naibu Katibu Mkuu wa CUF (Bara), Julius Mtatiro alisema mkutano huo utakaoanza saa 8 mchana hadi saa 12 jioni, utahudhuriwa na Profesa Ibrahim Lipumba wa CUF, Freeman Mbowe na Dk Willibrod Slaa wa Chadema, Mchungaji Christopher Mtikila wa DP na Dk Emmanuel Makaidi wa NLD.


Wengine ni Makamu wa Kwanza wa Rais wa Zanzibar, Maalim Seif Sharif Hamad, Mwenyekiti wa NCCR Mageuzi, James Mbatia, wawakilishi 10 kutoka kundi la 201 na wanachama mbalimbali kutoka umoja huo.


“Tunakwenda kuwaelimisha wananchi nini maana ya Katiba, jinsi ya kulinda maoni yao waliyoyatoa yasichakachuliwe na kuwaeleza kwa nini tuliamua kutoka bungeni,” alisema Mtatiro na kuongeza:


“Kesho (leo) tunafanya mkutano Unguja na keshokutwa (kesho) Pemba na tutatoa ratiba ya mikutano mbalimbali itakayofanyika Tanzania Bara kwa makundi tofauti.” Aprili 16 mwaka huu, Ukawa wakiongozwa na Profesa Lipumba walisusia Bunge la Katiba na kutoka nje kwa madai ya kutokuridhishwa na mienendo ya mjadala ya Bunge hilo.


Baada ya kutoka bungeni, walitangaza kufanya mikutano nchi nzima wakianzia Zanzibar.
 

TUCTA yawapigania wanafunzi..........


  TUCTA.png

  SHIRIKISHO la Vyama vya Wafanyakazi (Tucta), limeazimia kuendelea kupigania kushushwa kwa Kodi ya Mshahara (PAYE) kutoka asilimia 13 inayokatwa hivi sasa hadi asilimia tisa, ili mfanyakazi apate ahueni ya maisha.

Katibu Mkuu wa Tucta, Nicholas Mgaya, alisema hayo jana Dar es Salaam wakati akizungumzia maadhimisho ya Mei Mosi yatakayoambatana na wiki ya wafanyakazi itakayoanza rasmi leo.


Maadhimisho ya Mei Mosi yatafanyika nchini kesho kutwa ambapo kitaifa yatafanyikia jijini Dar es Salaam na mgeni rasmi atakuwa Rais Jakaya Kikwete.


Mgaya alisema mbali na kupunguzwa kwa kodi, Tucta inayo mambo mengine mawili inayopanga kupigania ili ujumbe ufike serikalini na kupatiwa suluhu.


Suala la pili alitaja kuwa ni kila mfanyakazi kupatiwa malipo mazuri awapo kazini, jambo alilosema wamekuwa wakiliomba mara kwa mara na hadi sasa halijakamilika.


“Kila mfanyakazi ni mstaafu mtarajiwa, hivyo ni vyema waajiri waandaliwe malipo mazuri, ili mfanyakazi atakapostaafu awe na kiwango cha maisha kitakachomsaidia katika maisha yake,” alisema Mgaya.


Pia wamejipanga kupigania mifuko ya pensheni, ilipe kiwango sawa cha kiinua mgongo tofauti na sasa ambapo baadhi ya mifuko inalipa kiwango kidogo na mingine inalipa kiwango kikubwa.


“Ifikie wakati sasa kusiwepo na utitiri wa mifuko, bali ivunjwe na kubaki miwili yaani wa binafsi na wa umma ambayo mengine yanabakia yakijitangaza tu,” alisema Mgaya.


Mgaya alilitaja jambo lingine kuwa ni fidia kwa wafanyakazi ambapo alishauri kuundwe kwa mfuko ambao utawezesha mfanyakazi atakayeumia kazini, kulipwa fidia ambayo itamsaidia.


Kuhusu mabadiliko ambayo yametokea tangu maadhimisho yaliyopita ya Mei Mosi, Mgaya alisema ni kupungua kwa kodi kutoka asilima 14 kwenda 13 ambayo alisisitiza kwamba wafanyakazi wanaomba sasa ifikie asilimia tisa

Jaji Warioba awalipua wanaomsaliti Mwl.Nyerere.................


Aliyekuwa Mwenyekiti wa Tume ya Mabadiliko ya Katiba, Jaji Joseph Warioba amesema wanasiasa wanaomtuhumu kwa kumsaliti Baba wa Taifa, Mwalimu Julius Nyerere kuhusu Muungano, ndiyo wasaliti kwa kuwa waliingiza kwenye Katiba, mambo yanayokinzana na makubaliano ya Muungano huo.

Jaji Warioba amesema usaliti huo ni pamoja na Serikali ya Mapinduzi Zanzibar kuondoa mamlaka ya Bunge la Muungano katika utungaji wa sheria, kuitambua Zanzibar kuwa nchi inayojitegemea na kuongeza mambo ya Muungano bila kufuata Katiba.


Ametoa kauli hiyo kujibu mwendelezo wa lugha za kejeli na matusi anazorushiwa na baadhi ya wajumbe wa Bunge Maalumu la Katiba wengi kutoka CCM na baadhi ya viongozi wa Serikali baada ya Tume aliyoiongoza kupendekeza muundo wa serikali tatu.


Akizungumza juzi usiku katika kipindi cha Dakika 45 kinachorushwa na Kituo cha Televisheni cha ITV, Jaji Warioba alisema viongozi wa pande mbili za Muungano wanaomtuhumu, ndiyo waliouvuruga Muungano huo


“Mwalimu aliacha Bunge likiwa na mamlaka kamili, aliacha nchi ni moja, aliacha mambo ya Muungano 11 sasa yamekuwa ni 22, kwa bahati nzuri Rais Jakaya Kikwete alieleza bungeni hilo kwamba mambo hayo yaliongezekaje,” alisema na kuongeza:


“Katika kubaini kuongezeka kwa mambo ya Muungano ndivyo ilikuwa inapunguza mamlaka kwa Zanzibar, mambo 11 yaliyoachwa na mwalimu yaliingizwa kikatiba lakini haya yaliyoongezeka yalipatikana kienyeji.”


Jaji Warioba alisema enzi za uhai wake, Mwalimu Nyerere aliheshimu na kuilinda Katiba hivyo, walioivunja ndiyo wasaliti wa Muungano.


“Sasa kati ya mimi na wao ni nani msaliti kwa Mwalimu, angekuwapo (Mwalimu) ni yupi angeonekana msaliti wa Serikali ya Muungano? Wao ndiyo wameuvuruga, alichokiacha Mwalimu ni tofauti na kinachoonekana kwa sasa,” alisema Jaji Warioba.


Kuhusu Bunge


Jaji Warioba alisema mipango mingi ya maendeleo inayopangwa ndani ya Bunge la Muungano inatekelezwa upande wa Bara pekee.


“Si hivyo tu, Bunge hilo linajadili mambo ya Bara tu na halihusishi upande wa Zanzibar. Zanzibar nayo inajadili mambo yake na kujiamulia lakini jina la Bunge hilo ni Muungano,” alisema Jaji Warioba.


Kutokana na mazingira hayo, Jaji Warioba alisema Zanzibar iliamua kuondoa mamlaka ya Bunge hilo katika utungaji wa sheria kupitia Baraza la Wawakilishi Zanzibar.


“Katiba ya Jamhuri ya Muungano inasema sheria zinazotungwa katika Bunge hilo zitatumika ndani ya pande zote za Muungano, lakini Zanzibar wakabadilisha hilo kupitia Katiba yao wakasema sheria zote zitakazotungwa ndani ya Bunge hilo, lazima zipitiwe tena na Baraza la Wawakilishi,” na kuongeza: “(Zanzibar) Hawakuishia hapo, wakafanya mabadiliko ya Katiba mwaka 2010 iliyovunja Katiba ikiitambua Zanzibar kama nchi kamili, ikaondoa mamlaka ya Rais wa Jamhuri kugawa wilaya na mikoa kwa Zanzibar tofauti na Katiba ya Muungano, kwa maana hiyo Zanzibar ikavunja nguvu ya Bunge la Muungano.”


Aidha, alisema hatua hiyo ilionekana kuuvunja Muungano kwa vitendo baada ya kuvunja mamlaka ya Rais na kutambua marais kamili katika nchi mbili tofauti.


“Kwa kawaida nchi inakuwa na amri jeshi mkuu mmoja ambaye anapigiwa mizinga 21, Jeshi la Muungano linapiga mizinga kwa marais wawili kitu ambacho hakiwezekani,” alisema.


Malalamiko ya Watanganyika


Jaji Warioba alisema Kwa upande wa Tanzania Bara, walibaini malalamiko ya Watanganyika kuwa ni pamoja na kukosa fursa mbalimbali ndani ya Zanzibar. “Watu wa bara nao wanasema Zanzibar inashiriki Bunge la Muungano, inakagua miradi ya bara na kuihoji lakini wao hawana nguvu ya kushiriki mambo hayo kwa upande wa Zanzibar,” alisema.


Aliongeza: “Mbaya zaidi wanasema Wazanzibari wanaweza kumiliki ardhi na kupata uraia kwa upande wa bara lakini haki hizo haziwezi kupatikana kwa Mtanganyika, njia pekee tukaona ni vyema Zanzibar nayo ilete mambo yake ndani ya Muungano lakini ikashindikana.”


Hoja ya takwimu


Jaji Warioba aliwataka wajumbe wa Bunge wasihangaike na takwimu badala yake wajibu maswali yaliyojitokeza kutoka kwa washirika wa Muungano.


“Takwimu siyo tatizo, sisi hatukufanya jambo jipya, ila ilikuwa ni kama marudio tu ya Tume ya Nyalali, wanahoji takwimu hizo je, hawakuona dosari kwa takwimu za maoni ya asilimia 20 kwa jaji Nyalali?


Alisema Tume yake ilizunguka nchi nzima ikiwa na waandishi waliorekodi kwa tepu, video na maandishi kwa ajili ya kuweka kumbukumbu katika mtandao wa Tume.

Basi lingine lapata ajali, laua 18..................


 
WATU 18 wamekufa papo hapo wakiwemo askari Polisi wanne katika ajali ya barabarani, wakati basi linalomilikiwa na Kampuni ya Sumry, lilipoparamia watu hao wakati wakimsitiri mtembea kwa miguu, aliyekufa kwa kugongwa na gari lisilofahamika.

Ajali hiyo ilitokea usiku wa kuamkia jana katika Kijiji cha Utaho, kilometa 20 nje ya Mji wa Singida katika Barabara Kuu ya Singida Dodoma.


Kamanda wa Polisi wa Mkoa wa Singida, Kamishina Msaidizi Mwandamizi, Geofrey Kamwela, alisema jana kuwa mbali na askari hao, wengine waliokufa papo hapo ni viongozi watatu wa kijiji hicho na wananchi wanaowaongoza na wengine wanne ambao hawajatambulika. 


Kwa mujibu wa Kamanda Kamwela, askari waliokufa katika ajali hiyo ni Koplo Boniface Magubika, PC Jumanne Mwakihaba, PC Novatus Tarimo na PC Michael Mwakihaba na wote wanatoka katika kituo kimoja cha kazi.


Viongozi wa Kitongoji na Kijiji cha Utaho waliokufa ni Ramadhan Mjengi, ambaye ni Ofisa Mtendaji wa Kijiji, Paul Hamis, ambaye ni Mwenyekiti wa Kijiji na Ernest Salanga ambaye ni Mwenyekiti Kitongoji.


Wananchi wanaowaongoza katika kijiji hicho waliokufa ni Saidi Rajabu, Ushirika Itambu, Chima Mughenyi, Salim Juma, Abeid Ramadhan, Mwinyi Hamis na Issaha Hussein.


Kwa mujibu wa Kamanda Kamwela, miili ya watu wengine wanne haikuwa rahisi kutambulika mara moja na wote wamehifadhiwa katika Hospitali ya Mkoa mjini Singida.


Kamanda Kamwela alisema ajali hiyo ilisababishwa na basi la abiria lenye usajili namba T.799 BET aina ya Nissan, mali ya Kampuni hiyo ya Sumry, inayomilikiwa na Mohamed Abdallah wa Sumbawanga, lililokuwa likienda jijini Dar es Salaam likitokea Kigoma.


Alisema kuwa basi hilo lililokuwa likiendeshwa na Paul Njilo, mkazi wa Dar es Salaam, liliwagonga waenda kwa miguu hao waliokuwa wamekusanyika kando ya barabara wakisaidiana na askari Polisi kuondoa mwili wa marehemu Gerald Zephania, aliyekuwa amegongwa na lori lisilofahamika juzi saa moja usiku.


Katika ajali hiyo kwa mujibu wa Kamanda Kamwela, watu wengine wanane walijeruhiwa na wamelazwa katika Hospitali ya Misheni Puma ya mjini Singida.


Habari kutoka eneo la tukio zinasema kilichosababisha ajali hiyo huenda ni kuegeshwa vibaya kwa gari la Polisi, wakati likipakia mwili wa marehemu Gerald, aliyekuwa amegongwa na lori mapema kabla ya basi hilo kufika hapo. Inadaiwa gari la Polisi liliziba barabara.


Akizungumzia ajali hiyo katika Makao Makuu ya Polisi Dar es Salaam jana, Kamishna Operesheni na Mafunzo wa Jeshi la Polisi, Paul Chagonja, alitoa pole kwa wananchi wote waliofiwa na ndugu zao na kuwaombea majeruhi kupona haraka.


Alisema Askari wa Usalama Barabarani hawatakuwa na muhali na dereva yeyote atakayekwenda kinyume na Sheria ya Usalama Barabarani. Kutokana na hilo, ametoa mwito kwa madereva kuzingatia sheria, kanuni na taratibu za usalama barabarni, ili kuepusha ajali zinazoweza kuzuilika.


“Polisi iko imara kuchukua hatua zozote za kisheria, kwani kuna baadhi ya watoa huduma wa usafiri hugoma pale wanapotaka kuchukuliwa hatua kwa sababu mbalimbali matokeo yake ni uvunjaji wa sheria kwa makusudi,” alisema.


Alisema Jeshi la Polisi limeanzisha msako mkali wa dereva wa basi hilo ambaye alitoroka ili kufikishwa mahakamani, na kuwaomba wananchi kuendelea kutoa ushirikiano kwa kutoa taarifa za wahalifu wa aina yeyote ile, ili wakamatwe na kufikishwa mahakamani. 

Diwani wa CCM kata ya Igalula,Tabora afariki dunia..........



Diwani Chama cha Mapinduzi (CCM) kata ya Igalula wilayani Uyui mkoa wa Tabora, Seleman Kapalu amefariki dunia kwa maradhi ya kifua. Taratibu za Mazishi zinaendelea.MUNGU AMLAZE ROHO YA MAREHEMU MAHALI PEMA PEPONI.…

Ingekuwa vizuri sana kama huu ushririkiano uliopo wa UKAWA ungekuwa ni wa kudumu.....


Bila shaka kila mwananchi anayeitakia mema nchi yetu amevutiwa na habari zilizochapishwa katika gazeti hili jana kwamba vyama vya siasa vinavyounda Umoja wa Katiba ya Wananchi (Ukawa), vimeamua kushirikiana katika Uchaguzi Mkuu wa 2015 kwa kusimamisha mgombea mmoja katika nafasi ya urais, ubunge na udiwani.

Viongozi wakuu wa vyama hivyo tayari wamekubaliana kuanza mchakato huo na wameandika mapendekezo na kuyapeleka katika sekretarieti za vyama vyao kwa ajili ya kufanyiwa uchambuzi.


Sisi tunaona kitendo hicho cha vyama vinavyounda Ukawa kuwa ni hatua muhimu ya kuongeza nguvu ili kuongeza ushindani ambao ni muhimu katika mustakabali wa nchi yetu kisiasa na hivyo kusaidia nyanja nyingine za kiuchumi na kijamii.


Tangu kuruhusiwa tena kwa siasa huru karibu miaka 22 sasa, bado nchi haijashuhudia ushindani wa kweli unaoweza kuwafanya watawala kuwajibika kwa wananchi kutokana na kuona hatari ya kuondolewa madarakani na vyama pinzani.


Hii imetokana na vyama shindani katika siasa kukumbwa na mifarakano ya kisiasa ambayo imekuwa ikiwagawa na hivyo kuingia kwenye chaguzi vikiwa dhaifu na hivyo kushindwa vibaya na chama tawala na matokeo yake yamekuwa ni wananchi wengi kukata tamaa na hivyo kusababisha idadi ya wanaoshiriki kupiga kura kupungua mwaka hadi mwaka kutokana na kutoona faida ya siasa za ushindani.


Pengine hiyo ndiyo sababu iliyofanya wananchi wapendekeze kwa Tume ya Mabadiliko ya Katiba kwamba vyama viruhusiwe kuunganisha nguvu wakati wa chaguzi kwa kuwa wameona bila ya nguvu ya vyama shindani, watawala wawataendelea kuongoza kwa mazoea na matokeo yake ni wananchi kuendelea na umaskini wao na kuona uhuru wa vyama vya kisiasa hausaidii kuwa kuboresha maisha yao.


Si nia yetu kuona chama tawala kikiondolewa madarakani na vyama shindani, lakini tunachotaka kuona na ushindani wa dhati, makini na wa kweli ambao, kwa taifa lolote lile, ni afya kwa ustawi wa wa taifa kwa kuwa huongeza uwajibikaji kwa watawala.


Hakuna ubishi kwamba upinzani wenye nguvu huisukuma serikali ichape kazi na kuwatumikia wananchi kwa kutambua kwamba ikiboronga itaondolewa madarakani na serikali kivuli ambayo ni vyama vya upinzani.


Vyama legelege vya upinzani huogopa kivuli cha serikali na kufifisha maendeleo na kuzima matumaini ya wananchi wanaotaka kuona uwajibikaji serikalini, kwani huwa chachu ya kuendeleza tawala za kiimla zisizothamini demokrasia na zisizowajibika kwa wananchi.


Ndiyo maana tunawapongeza viongozi wa Ukawa kwa kuona umuhimu wa kuunganisha nguvu na kuwa wamoja ili kuweka ushindani wa kweli katika mazingira ya kisiasa tuliyomo.


Tunachoweza kuwashauri viongozi wa Ukawa ni kuwa makini na kuondoa tofauti zinazowatenganisha. Ukawa isitarajie kwamba kila kitu kitakuwa mteremko, kwani bado sheria kandamizi ambazo zimekuwa zikikwaza shughuli za upinzani bado hazijafutwa.


Ni matarajio yetu kwamba serikali na chama tawala kitachukulia hatua hiyo ya Ukawa kuwa changamoto ya kuongeza ufanisi katika kuwatumikia wananchi na si kuanza kujenga chuki na kutafuta mbinu za kuikwamisha.

Unakijua alichokisema Guardiola baada ya kupokea kipigo kutoka kwa Mdrid jana.........fuatilia hapa.

397592_heroa
PEP Guardiola ameeleza kuwa kiwango walichoonesha Bayern Munich ni kikubwa mno japokuwa walifungwa mabao 4-0 na Real Madrid katika mchezo wa nusu fainali ya pili ya UEFA kwenye uwanja wa Allianz Arena jana.
The Bavarians walichanganyikiwa kwa mabao mawili ya Sergo Ramosi na Cristiano Ronaldo na kuvuliwa ubingwa kwa wastani wa mabao 5-0 kufuatia kupigwa bao 1-0 mchezo wa kwanza Santiago Bernabeu.

Guardiola ambaye kikosi chake kilicheza kwa kujituma zaidi katika kipigo cha kwanza cha bao 1-0 Bernabeu, hakikuweza kufua dafu jana Allianz Arena.

“Kila kitu kinatokea katika mpira kutokana na kucheza vizuri. Nimefungwa mara nyingi katika kazi yangu na hii ni mojawapo”. Guardiola amewaambia waandishi wa habari.

“Tulifungwa mabao mengi, lakini tulicheza kwa kiwango kikubwa na ndio sababu ya kupoteza”.

“Hakuna sababu nyingine, huu ndio mpira”.

“Unapocheza vibaya, unafungwa mabao mengi. Tuliingia na nguvu, tungeweza kufunga kwa nafasi tulizopata, lakini hatukuweza”.

“ Kucheza kwetu vibaya ndio sababu pekee ya kufungwa”.

Bayern imefanikiwa kutwaa kombe la dunia la klabu na Bundesliga msimu huu, na wamebakiwa na kombe la mwisho la DFB-Pokal mei 17 dhidi ya Borussia Dortmund.

Hii itakuwa kama marudio ya fainali ya ligi ya mabingwa barani Ulaya mwaka jana

Adnan Januzaj ahakikishiwa nafasi Ubelgiji katika fainali za kombe la dunia Brazil...

ADNAN_JANUZAJ-IN_RED


















CHIPUKIZI wa Manchester United, Adnan Januzaj, atakuwemo kwenye Kikosi cha awali cha Kombe la Dunia cha Belgium kama ilivyohakikishwa na Kocha wa Nchi hiyo Marc Wilmots.
Wiki iliyopita, Marc Wilmots ndie alietoboa kuwa Januzaj amekubali kuichezea Belgium licha ya kutakiwa na kuwa na uwezo wa kuziwakilisha Albania, Kosovo, Turkey na Serbia kwa misingi ya mizizi ya Asili ya Wazazi wake.
Januzaj atakuwemo kwenye Timu ya Belgium ambayo itapiga Kambi ya Mazoezi Mwezi ujao kujitayarisha na Fainali za Kombe la Dunia zitakazochezwa huko Brazil kuanzia Juni 12 lakini Kocha Marc Wilmots amesema hivi sasa hawezi kuahidi kama Kinda huyo atakuwemo kwenye Kikosi cha mwisho cha Wachezaji 23 watakaoenda Brazil.
Kocha huyo amesema: “Nimemuona mara kadhaa akicheza na sasa nataka kumuona akiwemo kwenye Kikosi changu. Atakuwemo kwenye Kikosi cha Awali cha Wachezaji 30 na atakuwepo kwenye Kikosi cha Wachezaji 26 au 27 ambao watafanya Mazoezi huko Genk na baadae Sweden. Napenda kuwa na idadi ndogo ya Wachezaji lakini Januzaj atakuwemo.”
Januzaj, mwenye Miaka 19, alijiunga na Manchester United Mwaka 2011 akitokea Anderlecht na Msimu huu amepandishwa na kuwemo Kikosi cha Kwanza cha Timu hiyo na Mechi yake ya kwanza ilikuwa ya Ngao ya Jamii ambayo Man United waliibwaga Wigan 2-0 Mwezi Agosti Uwanjani Wembley.
Tangu wakati huo amecheza Mechi 32 na kuifungia Man United Bao 4.
Kocha Wilmots alifafanua kuwa alipokutana na Januzaj  na Mawakala wake aliwaambia wazi kuwa uamuzi wa Mchezaji huyo kuwemo kwenye Kikosi kitakacho kwenda Brazil kitategemea nini atafanya Uwanjani lakini alidokeza kuwa kuumia kwa Christian Benteke kumezidisha nafasi yake kucheza Kombe la Dunia.
Wilmots amesema: “Kwa hakika huyu ni Mchezaji wa kuvutia na hasa baada kukosekana Benteke. Watu wengi hawajui kuwa akiwa na Timu ya Rizevu ya Manchester United mara nyingi amecheza kama Namba 9. Kumudu kwake nafasi nyingi ni mali!”

Real Madrid yaivua rasmi Bayern Munich Ubingwa UEFA ....yawapiga 5-0.......

BAYERN Munich wamevuliwa ubingwa wa UEFA kwa kipigo cha mbwa mwizi baada ya kufungwa mabao 5-0 na Real Madrid katika mechi mbili za nusu fainali ya ligi ya mabingwa barani Ulaya.
Mechi ya kwanza katika dimba la Santiago Bernabeu, Real Madrid walishinda bao 1-0 na leo hii katika nusu fainali ya pili kwenye uwanja wa Allianz Arena mjini Munich, kikosi cha Carlo Ancelotti kimeibuka na ushindi wa mabao 4-0.

Real Madrid walitumia dakika 16 tu kufunga goli ambapo Luca Modric alichonga kona kutoka winga ya kulia na Sergio Ramos kujitwishwa mpira huo na kuuzamisha kimiani.

Dakika nne baadaye, beki huyo wa kati aliwamaliza Bayern baada ya kuunganisha kwa kichwa mpira wa adhabu ndogo uliochongwa na Gareth Bale.
article-0-1D74992A00000578-72_634x423Baadaye Real Madrid walifanya shambulizi la kushitukiza ambapo Cristiano Ronaldo alifunga bao safi baada ya Bale kumpatia pasi murua.

article-0-1D74970700000578-13_634x445 
Bao hilo liliwafanya Real wahitimishe dakika 45 za kipindi cha kwanza kwa mabao 3-0.
Bao la dakika ya 90 la Cristiano Ronaldo kwa njia ya adhabu ndogo lilitia chumvi katika kidonda cha Bayern na kuvuliwa ubingwa kwa wastani wa mabao 5-0.

Kabla ya mechi hii, nyota wa zamani wa soka la Ujerumani, Stefan Effenberg alionesha wasiwasi wake kama falsafa ya Pep Guardiola itaisaidia Bayern Munich kutwaa ubingwa wa UEFA, wakati huu ambapo mchezaji muhimu Frank Ribery yupo katika kiwango cha chini.

Effenberg anaamini falsafa ya sasa ya Bayern ya kupiga pasi nyingi haikuweza kuwasaidia Bernabeu na alikuwa na wasiwasi katika mechi ya leo.

Kipigo cha mabao 4-0 kimethibitisha mawazo ya gwiji huyo wa soka la Ujerumani.
article-0-1D74811C00000578-501_634x452Tangu enzi za Zinedine Zidane, Luis Figo, Roberto Carlos na Raul, Real Madrid hawajacheza fainali na sasa wamefanikiwa kuelekea La Decima mjini Lisbon mwezi ujao.
Kabla ya mechi, watu walikuwa wanasema Real Madrid wanahitaji bao 1 zaidi au suluhu ili kuwashinda Bayern, lakini wameweza kushusha mvua kubwa ugenini.

Baada ya mechi hiyo, Gareth Bale amesema kipigo walichotoa leo hii ni sababu mojawapo ya yeye kujiunga na klabu kubwa duniani majira ya kiangazi mwaka jana.

“Ni matokoe mazuri mno kwetu. Nadhani tumejituma, tulitumia vizuri mbinu zetu na kucheza vizuri usiku huu, hivyo tulistahili ushindi”. Bale amezungumza na ITV.

“Walicheza mpira sana, waliacha nafasi za kushambuliwa kwa kushitukiza, nasisi tunapenda hivyo”.

“Tuna wachezaji wenye kasi na tunatumia nafasi kama hizo. Tulikuwa katika kiwango bora na tumefurahi kufika fainali”.

“Lakini kuna hatua nyingine mbele”.

“Kiukweli hii ndio sababu ya kwanini nilijiunga na Madrid. Ndio maana niliamua kuja kujiunga na klabu kubwa zaidi duniani”

“Lengo ni kushinda makombe na mechi kubwa. Tunatakiwa kushinda taji, tutakuwa na fainali ngumu kwa timu yoyote itakayopita kesho”.
article-2616240-1D74F53100000578-959_634x429Ronaldo baada ya kufunga mabao mawili usiku huu amevunja rekodi ya Lionel Messi kwa kufikisha mabao 16 katika msimu mmoja wa UEFA.


 

Real Madrid wamefuzu kwa mara ya kwanza fainali tangu walipofanya hivyo mwaka 2002 na kutwaa kombe na sasa wanatarajia kukutana na Chelsea au Atletico Madrid ambazo zitapambana kesho katika uwanja wa Stamford Bridge.
Mechi ya kwanza katika dimba la Vicente Calderon mjini Madrid, Chelsea walilazimisha suluhu ya bila kufungana, hivyo wanahitaji bao 1-0 ili kufuzu fainali

£830million zatumika kuutafuta ubingwa Ulaya.............


article-2615739-059DB279000005DC-440_634x394
 
Tangu mwaka 2002 wakati Zinedine Zidane alipofunga moja ya magoli mazuri kabisa katika historia ya Champions League na kuiwezesha Real Madrid kutwaa wa ulaya kwa mara ya mwisho mpaka leo – klabu hiyo ya Hispania imetumia zaidi ya £830million kwa ajili ya usajili wa wachezaji mbalimbali ili kuweza kutimiza ndoto yao ya kuwa timu ya kwanza ya ulaya kufikisha idadi ya makombe 10 ya ulaya. WACHEZAJI WALIOSAJILIWA NA MADRID KATIKA KULISAKA KOMBE LA 10 LA ULAYA:
02/03
Ronaldo (Inter) £20m
03/04
David Beckham (Man Utd) £25.5m
04/05
Walter Samuel (Roma) £16.7m
Michael Owen (Liverpool) £8m
Jonathan Woodgate (Newcastle) £13.4m
Antonio Cassano (Roma) £5m
Thomas Gravesen (Everton) £2.5m
05/06
Cicinho (Sao Paolo) £3.5m
Robinho (Santos) £20m
Julio Baptista (Sevilla) £16.9m
Sergio Ramos (Sevilla) £22m
06/07
Ruud van Nistelrooy (Man Utd) £11m
Mahamadou Diarra (Lyon) £21m
Fabio Cannavaro (Juventus) £6m
Emerson (Juventus) £26m
Christoph Metzelder (Dortmund) Free
Wesley Sneijder (Ajax) £22.7m
Javier Saviola (Barcelona) Free
Roysten Drenthe (Feyenoord) £11.5m
07/08
Gabriel Heinze (Man Utd) £8m
Arjen Robben (Chelsea) £24m
08/09
Rafael van der Vaart (Hamburg) £11.4m
Lassana Diarra (Portsmouth) £20m
Klaas-Jan Huntelaar £20m
09/10
Kaka (Milan) £56m
Cristiano Ronaldo (Man Utd) £80m
Karim Benzema (Lyon) £25m
Alvaro Arbeloa (Liverpool) £3.5m
Xabi Alonso (Liverpool) £30m
10/11
Angel Di Maria (Benfica) £29m
Sami Khedira (Stuttgart) £11.5m
Sergio Canales (Racing) £4m
Ricardo Carvalho (Chelsea) £6.7m
Mesut Ozil (W Bremen) £12.4m
11/12
Nuri Sahin (Dortmund) £8m
Jose Callejon (Espanyol) £5.5m
Fabio Coentrao (Benfica) £25.5m
Raphael Varane (Lens) £11.5m
12/13
Luka Modric (Spurs) £33m
Diego Lopez (Sevilla) £3m
13/14
Isco (Malaga) £23m
Asier Illarramendi (Sociedad) £34m
Gareth Bale (Spurs) £85.3m
Daniel Carvajal (Leverkusen) £5m

Ashtakiwa kwa kuzinyofoa nyeti za mumewake kisa wivu na ugomvi wa kimapenzi..........

 









 Jeshi la polisi mkoa wa Pwani linamshikilia Husna Iddi Kisoma (19) , mkazi wa Kisemvule Mkuranga mkoa wa Pwani kwa tuhuma za kumuua mumewe Jumane Mwalami (21) baada ya kumvuta sehemu za siri na kuzinyofoa kutokana na ugomvi uliosababishwa na wivu wa mapenzi.

 Akizungumza na kipindi cha Maskani cha 100.5 Times Fm, kamanda wa Polisi mkoa wa Pwani, Ulrich Matei ameeleza kuwa tukio hilo lilitokea juzi usiku na kwamba kulikuwa na ugomvi kati ya wawili hao huku kijana huyo akimtuhumu mwanamke huyo kuwa na uhusiano wa kimapenzi na wanaume wengine.

 Ameeleza kuwa wakati ugomvi unaendelea, mwanamke huyo alizishika sehemu za siri za mumewe na kuzivuta hadi kuzinyofoa.

Mwanaume huyo alipata maumivu makali na alikimbizwa hospitali ya Mkulanga ambapo alifariki.


Jeshi la polisi limefanikiwa kumkamata mtuhumiwa huyo na tayari ameshafikishwa mahakamani akikabiliwa na kesi ya mauaji.

Tazama hii picha ambayo wame-edit Rais Kenyatta akimuangalia askari mwenye hips za kudatisha..............

 

Mtu Mzima ni kama aamini anacho kiona....."Aisee huyu mleteni awe board guard wangu ...Life is Good.....hahah

Askari mwenye hips za kupagawisha Kenya achimbwa mkwara na bosi wake.........

 
Yule Polisi Mwanamke Nchini Kenya kwa Jina Linda Amechimbwa mkwara na Bosi wake wa kituo cha Polisi kiambu Kenya Baada ya Picha yake Kusambaa Mitandaoni Akiwa amevaa Kijisketi cha Polisi kinacho mchora Hips na makalio yake kiasi cha kuleta utata kwenye mitandao ya kijamii kwa kusababisha Mjadala usio na Mwisho kila mtu akisifia hips na kalio lake..Vipi we Mwanamme, Trafiki kama huyu akikusimamisha Barabarani ? Najua lazima uchukue Number ya Simu hahahha

Wachezaji Mbeya City wazuiwa kuhama timu........


WAKATI klabu kongwe za Simba, Yanga na Azam FC zikipiga hesabu za kuibomoa Mbeya City, Serikali imewaonya wachezaji hao kukihama kikosi hicho kinachofundishwa na Juma Mwambusi.

Zipo tetesi tofauti za wachezaji wa timu hiyo iliyomaliza ligi ikiwa katika nafasi ya tatu katika ligi kuwaniwa vikali na klabu hizo kwa ajili ya msimu ujao wa Ligi Kuu Bara.


Akizungumza na Mwanaspoti, Mwenyekiti wa timu hiyo, Mussa Mapunda alisema Aprili 24, mwaka huu walipokea barua kutoka Wizara ya Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo iliyosainiwa na Naibu Waziri, Juma Nkamia ikiwasisitizia jambo hilo.


“Barua tuliyoipokea iliandikwa Aprili 15 kabla ya sisi kuipokea Aprili 24, ambayo imeelekeza kuendelea kuwapa matunzo mazuri wachezaji wetu wote bila ya kubagua kwa lengo la kukiboresha kikosi chetu ili msimu ujao kiimarike zaidi.


“Imetuonya kutowaruhusu wachezaji wetu kuwaachia kwenda klabu kubwa ambazo zenyewe hazina malengo na mpangilio wa kuziendeleza timu zao,”alisema Mapunda.


Wachezaji wanaotajwa kuwaniwa na klabu za Simba, Yanga na Azam FC ni Saad Kipanga, Hassan Mwasapili na Deus Kaseke.

Inasikitisha sana:Trafiki kafa ghafla akiwa kwenye daladala aliyoikamata............


Moshi. Ofisa wa polisi mwenye cheo cha Koplo, Wilson Mwakipesile wa Kikosi cha Usalama Barabarani mkoani Kilimanjaro amefariki dunia ghafla akiwa ndani ya daladala alilokuwa amelikamata.


Hata hivyo, haikujulikana mara moja iwapo trafiki huyo alifariki dunia akiwa njiani kulipeleka gari hilo kituo cha polisi, alifariki muda mfupi baada ya kufika kituoni au wakati anapelekwa hospitali.


Kamanda wa Polisi Mkoa wa Kilimanjaro, Robert Boaz alisema polisi huyo alikufa ghafla akiwa kazini lakini alikataa kuingia kwa undani wa tukio hilo lilitokea Ijumaa kati ya saa 5:00 asubuhi na saa 6:00 mchana, baada ya trafiki huyo kukamata daladala linalofanya kazi zake kati ya Kiborloni na katikati ya mji.


Mmoja wa mashuhuda alisema “Baada ya kuikamata hiyo Hiace (Toyota) pale Kiborloni aliingia kwenye hiyo gari na kukaa kiti cha mbele pembeni ya dereva na kumwamuru kulipeleka kituoni.


“Wakati wakiwa njiani kuelekea kituoni ghafla yule trafiki akawa haongei na akawa anamwegemea dereva… hiyo hali iliendelea hadi walipofika kituoni ndipo dereva akawaeleza trafiki wenzake.” Mwili wa polisi huyo ulisafirishwa juzi kwenda Mbeya kwa mazishi.

Tuesday, 29 April 2014

Je unazijua aina za vitambi....fuatilia hapa....!!!!!

 
1. Kitambi Mvurugo -- hiki kitambi kimekaa kama O.
Kinapatikana kwa kula sana kitimoto.

2. Kitambi Mchuchumio -- hiki kitambi kimekaa kama
herufi D. Kinatokana na kula sana michemsho na bia za
ofa.

3. Kitambi Mbonyeo -- Akivua shati kitovu hakionekani.
Hiki wanacho wala rushwa. Ila akisimamishwa kazi
kinaisha.

4. Kitambi Mtepeto -- Ni kitambi cha wastani ambacho
ukivaa nguo pana
hakionekani. kinasababishwa na kula mno viporo.

5. Kitambi Mfumanio: hiki mtu anakuwa hana pesa ila
kitambi ni kutokana na minyoo na utapiamlo wa ukubwani.

6. Kitambi Mtunguo: Hiki wanacho sana wadada. Kina
umbo la yai. Hiki kwa 'diet' hakitoki labda Kwa Maombi tu

Mwanachuo afia chumbani kwa hawara yake...........




MSICHANA Atu Gabriel mwenye umri wa miaka 20,  mwanafunzi wa Chuo cha Eden Hill kilichopo Kwamfipa wilayani Kibaha mkoani Pwani, amekutwa amekufa chumbani kwa mtu anayetajwa kuwa ni hawara yake, Hafidh Mohammed.


Tukio hilo lilitokea April 26, mwaka huu na kukusanya umati huku mwanaume aliyelala na binti huyo akitokomea kusikojulikana.Marehemu anadaiwa kuwa mwenyeji wa Makambako mkoani Njombe.


Akizungumza na waandishi wetu juzi Kibaha, mama wa Hafidh ambaye pia ni mjumbe wa eneo hilo, Zainabu Saidi alisema mwanaye alimweleza kutokea kwa tukio hilo asubuhi kulipokucha na kabla ya hapo, hakuwa akifahamu kama alikuwa na uhusiano wa kimapenzi na msichana huyo kwa vile aliyekuwa akimfahamu ni mwanamke mwingine ambaye alizaa naye.


“Mimi kwa kweli sikuwa na taarifa yoyote juu ya uhusiano wao na huyu  mwanafunzi, nimeletewa taarifa asubuhi na kijana wangu huku akionekana kuchanganyikiwa, nimejaribu kumsihi asikimbie lakini imeshindikana,” alisema mama huyo.


ALIVYOAGA CHUONI

Wanafunzi wa chuo hicho kinachofundisha masomo ya biashara na habari ambao walikataa kutaja majina yao waliliambia gazeti hili kuwa, marehemu Atu aliwaaga anakwenda jijini Dar es Salaam kumuuguza wifi yake aliyelazwa katika Hospitali ya Amana, Aprili 23, mwaka huu.


Hata hivyo, walisema uondokaji wake uliwapa maswali mengi kwani tofauti na walivyotegemea kuwa angebeba mfuko mkubwa wenye nguo za kubadili, yeye aliondoka akiwa na mkoba wake wa mkononi pekee hali iliyoonesha hakuwa akienda mbali.


Walisema siku tatu baadaye walipatwa na mshtuko mkubwa baada ya mlinzi wa hosteli yao kuwaletea taarifa za kifo cha mwenzao kilichotokea katika chumba cha mvulana huyo anayeishi jirani.


MAJIRANI NAO WANENA

Majirani waliozungumza na gazeti hili walisema kwao haikuwa mara ya kwanza kumuona msichana huyo, kwani mara kwa mara alikuwa akifika pale ingawa akishaingia ndani hakuwa akitoka nje.


Walisema mara zote hizo, mwanaume huyo mwenyeji ndiye alikuwa akitoka nje na kwenda kumnunulia chakula.


POLISI WAUPELEKA MWILI HOSPITALI YA TUMBI

Jeshi la polisi liliwasili eneo la tukio na kuukuta mwili huo ukiwa umelala kitandani ukiwa hauna jeraha, lakini pembeni yake kulikutwa vidonge ambavyo havikufahamika ni vya aina gani ambavyo pia vilichukuliwa pamoja na mkoba wake hadi kituonis.


Minong’ono kutoka kwa majirani kuhusiana na vidonge hivyo ilitofautiana,  baadhi yao walisema huenda vilitumika katika jaribio la kutoa mimba, wengine walisema inawezekana msichana huyo alipata ugonjwa wa ghafla usiku na mwanaume huyo alikwenda kumchukulia vidonge hivyo ambavyo havikuweza kumsaidia marehemu kupata nafuu.


Kamanda wa Polisi Mkoa wa Pwani,  SACP Ulrrich Matei alithibitisha kutokea kwa tukio hilo na kusema juhudi za kumtafuta mwanaume huyo zinaendelea huku madaktari nao wakiendelea na uchunguzi wao ili kubaini chanzo cha kifo hicho

Mbowe kaja na Plan B ni nodari sana.....


Katika kikao kimoja tulichofanyia Mwanza mwaka jana mwishoni Mbowe aliwakuna wajumbe alipotupa siri kwamba alikataa kuwa mwenye kiti wa Chadema mpaka kamati kuu walipokubali mashariti yake. Baadhi ya mashariti ilikuwa kumuomba na kamati kuu ikubali Dr Slaa awe Katibu mkuu badala ya makamu mwenyekiti, kuruhusu kufungua milango ili aingize watu toka vyama vingine na kubadilisha rangi za bendera ya chama. Alitwambia jinsi alivyopata shida kuwashawishi wazee wa chama kukubali kombati kuwa vazi la chama na kadhalika. Ilikuwa story ya kuvutia sana!

Leo wakati Ccm wakidhani tuna tofauti kubwa sana na vyama vingine hasa Cuf, na walijitahidi sana kupanda chuki kati yetu. Na zaidi walijitahidi kuivuruga Chadema kwa kutumia mamluki, kumbe Kamanda wa anga anafikiria kitu kikubwa zaidi. Ametoka na plan B amabayo inawafanya Ccm warudi kwenye drawing board kupanga upya mbinu tofauti na hii ya mamluki. Kwa vyovyote sasa mbinu ni kuchonganisha huu muungano maana hauwezi kuwaacha salama.


Mchambuzi yoyote wa siasa anajua kwamba tukiingia kwenye uchaguzi kwa muungano huu Ccm watatoka jasho kweli kweli. Muungano huu utasambaratisha kabisa propaganda ya udini na ukabila, utasambaratisha propaganda ya uchu wa madaraka. Lakini italigawa taifa katika kanda ambazo ni rahisi kupiga kampeini kulingana na sehemu vyama vinavyokubalika. Itapunguza mzigo wa gharama maana utashughulikia eneo dogo kwa ufanisi.


Endelea kutembelea katemimethsela.blogspot.com uweze kujua kitakachojiri.....

Alves awakomesha wabaguzi..................

Asee Dan Alvez n bonge la jembe kuna mshabiki kamrushia ndizi ye kaichukua kaimenya afu akaila huyooo akaendelea kupiga kona....inaitwa komesha ubaguzi...

THIS IS THE BEST FOOTBALL QUOTE EVER‪
Dani Alves-"I don't know who it was, but thanks to whoever threw the banana, the potassium gave me the energy for the two crosses which led toa goal,"
Dani alves amepata support kutoka kwa wachezaji wenzake wa timu ya taifa ya Brazil pamoja na Sergio Aguero na Mata ...SAY NO TO RACISM
 
 

Basi la Hood laungua vibaya Chalinze................

 

Zaidi ya Abiria 55 waliokuwa ndani
ya Basi la kampuni ya Hood,
wakisafiri kutoka Mbeya kwenda
Arusha walinusurika kufa baada ya
Basi hilo kushika moto na
kuteketea kabisa katika kijiji cha
Kilolele-Chalinze Mkoani Pwani.

Breaking News:Kavumbagu atua azam......


Na Mahmoud Zubeiry, Dar es Salaam
NAHODHA wa Burundi, Didier Kavumbangu
amesaini Mkataba wa miaka miwili na mabingwa
wapya wa Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara,
Azam FC mchana wa leo, BIN ZUBEIRY imeipata
hiyo.
Kavumbangu aliyemaliza Mkataba wake wa
miaka miwili Yanga SC, ameamua kusaini Azam
FC baada ya kuona klabu yake haina
mawasiliano naye licha ya kumaliza Mkataba
wake.
“Mimi ni mchezaji, kazi yangu ni mpira.
Nimemaliza mkataba Yanga, lakini viongozi
hawaniambii kitu, nimepata ofa nzuri Azam
nikaamua kusaini,” amesema Kavumbangu
akizungumza na BIN ZUBEIRY baada ya kusaini
Mkataba huo ambao unamfanya alipwe vizuri
kuliko alivyokuwa analipwa Jangwani.
Pamoja na hayo, Kavumbangu ameishukuru
Yanga SC na mashabiki kwa miaka miwili
aliyoichezea timu hiyo na anasema itabakia
kwenye kumbukumbu zake kwa ameshinda nayo
mataji.
Mshambuliaji huyo mrefu mwenye nguvu
amesema sasa akili yake anaipeleka kwa mwajiri
wake mpya, Azam FC ambako pia amepania
kwenda kushinda mataji na kuiwezesha timu hiyo
ya Alhaj Sheikh Said Salim Awadh Bakhresa na
familia yake kufanya vizuri kwenye michuano ya
Afrika.
“Mimi sasa ni mchezaji wa Azam, nafurahi
kujiunga na klabu hii kubwa. Kawaida yangu
huwa nashabikia klabu nayochezea, sasa mimi ni
mshabiki namba moja wa Azam,”amesema.
Kavumbangu alitua Yanga mwaka 2013 akitokea
Atletico ya Burundi na katika mechi misimu
miwili ya kuichezea klabu hiyo, amefunga mabao
31 katika mechi 63 za mashindano yote, moja tu
la penalti.
Maisha mapya; Kavumbangu akitia dole gomba
Mkataba wa Azam leo
Tukutane Chamazi; Kavumbangu anahamisha
virago vyake kutoka Jangwnai hadi Chamazi

Muslim Brotherhood latangazwa kama kundi la kigaidi nchini Misri.............

Wafuasi wa Muslim Brotherhood

Serikali ya kijeshi ya Misri imetangaza kuwa chama cha Muslim Brotherhood ni kundi la kigaidi.
Uamuzi huo umetangazwa na Naibu Waziri Mkuu,Husam Muhammad Isa.
Serikali imekilaumu chama hicho kwa shambulio la bomu lilofanywa Jumaane dhidi ya makao makuu ya polisi katika mji wa Mansoura, kaskazini ya Cairo ambalo liliuwa watu 13.
Imesema kuwa maandamano yote yatayofanywa na chama hicho ni kinyume cha sheria na mtu yeyote anayependekeza chama hicho atapewa adhabu.
Mwandishi mmoja mjini Cairo anasema Muslim Brotherhood imepigwa marufuku kwa miongo kadha na tangazo la sasa linachukua hatua zaidi - inamaanisha kuwa fedha na mali yote ya chama hicho sasa inaweza kutaifishwa.