Sunday, 27 April 2014
Kujichubua ngozi ni tatizo kwa mastaa wetu...angalia hapa baadhi......
Unaweza kuamini ukiambiwa kuwa, umaarufu hapa Bongo unakuja na rangi yake ya kipekee, hata kwa watu wanaochipukia na kutamani kuwa maarufu siku moja, wanaamini kuwa, ili kufanikiwa ni lazima kwanza uwe na rangi nyeupe ya ngozi yako, huwezi kushangaa kwa hili sababu hata Lupita Nyong’o pamoja na kufanikiwa kuwa mwanamke mwenye mvuto mwaka 2014, naye alikuwa anaamini hilo alivyokuwa mdogo.
Hapa kwetu Bongo imekuwa kama ugonjwa vile wa kuambukizwa kati ya watu maarufu na hata wale wanaochipukia, kujikuta wanatumia kila hali kubadilisha ngozi yao, wapo wasanii wengi sana na watu maarufu, ambao hutoweza amini uonapo jinsi walivyokuwa hapo nyuma na hivi sasa wanavyoneka, kama ulikuwa hujui hili ni kwamba endapo mtu akibadilika namna hii, ni vigumu kabisa kurudi hali yake ya zamani ya uhalisia.
Watu Wengi maarufu wamejikuta wakijutia kujibadili haswa pale miaka inavyozidi kwenda, kutokana na madhara yanayo wakumba kwenye ngozi zao hizo, kwa asilimia kubwa madhara yake yanatibika, ila pesa yake ya matibabu ni ndefu, jambo ambalo ni cost kubwa sana kuanza kujitibu ni bora kujiepusha kabisa na mambo hayo ya urembo wa muda.Hizi ni baadh tu ya picha za wasanii wetu wa hapa Tzee ambao hutoweza amini jinsi walivyobadilika, kabla na baada ya kupata umaarufu.
Wema Sepetu.
Ray-C.
Diva Loveness.
0 comments:
Post a Comment